Home Kimataifa Kilichojiri hii leo dunia nzima, fainali klabu Afrika hakuna mbabe

Kilichojiri hii leo dunia nzima, fainali klabu Afrika hakuna mbabe

3756
0
SHARE

Pale nchini Misri fainali ya kwanza ya michuano ya klabu bingwa Afrika ilipigwa huku wenyeji Al Ahly wakilazimishwa suluhu ya bao moja kwa moja, walianza Ahly dakika ya 3 kupitia Momen Zakaria kabla ya Benchargui kusawazisha.

Nchini Italia kulipigwa mtanange mkubwa kati ya Ac Millan waliokuwa nyumbani wakiikaribisha Juventus na Gonzalo Higuain akawaumiza Millan kwa kuwapiga bao mbili huku wao wakitoka kapa.

Manchester United wameweka rekodi kama timu pekee kutoruhusu goli nyumbani huku Anthony Martial akiwa ndio mchezaji anayetokea sub anayeongoza kwa idadi ya mabao barani Ulaya baada ya leo kufunga bao pekee dhidi ya Tottenham.

Manchester City waliichapa West Bromich bao 3 kwa 2 na kuipa klabu hiyo rekodi pekee ya kushinda michezo 6 ya ugenini mfululizo, ushindi ambal umezidi kuwaweka katika kilele cha Epl

Bao pekee la Eden Hazard limewafanya Chelsea kushinda michezo tisa kati ya kumi na moja zilizopita ambayo wamecheza katika viwanja vya ugenini.

Katika matokeo mengine Arsenal wameipiga Swansea City bao mbili kwa moja huku Liverpool wakiipiga Hudddersfield mabal 3 kwa moja.

Ujerumani balaa limeendelea kuwakumba Borussia Dortmund baada ya leo kupigwa bao 4 kwa 2 na Hannover 96 huku Borussi Dortmund wakimaliza 10 uwanjani baada ya Axel Zagadou kupewa kadi nyekundu.

Wakati Borussia Dortmund wakichezea kipigo hicho, mahasimu wao wakubwa klabu ya Bayern Munich wameendelea kutakata baada ya hii leo kuwachapa Rb Leizp kwa mabao mawili ya James Rodriguez na Roberto Lewandoski.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here