Home Ligi EPL Man Utd vs Spurs: Mourinho na Mnyonge wake Pochettino, DeGea vs Lloris,...

Man Utd vs Spurs: Mourinho na Mnyonge wake Pochettino, DeGea vs Lloris, Kane, Pogba OUT!!

7410
0
SHARE

Kwa mara ya kwanza ndani ya takribani kipindi cha mwezi, United watarejea nyumbani Old Trafford wikiendi hii kukipiga dhidi ya Spurs. Mchezo huu unazikutanisha timu zinazoshika nafasi ya pili na ya tatu, ambazo zote zina pointi 20 baada ya mechi 9.

Timu zote zimekuwa na matokeo tofauti kwenye michuano ya Carabao Cup, na wanafahamu pointi 3 zinaweza kuwasogelea Manchester City ambao wana pointi 25.

Manchester United

Kufuatia michezo 4 mfululizo ugenini katika mashindano tofauti, Mashetani Wekundu wanarejea Old Trafford kwa mara ya kwqnza tangu walipowafunga Crystal Palace 4-0, September 30, wakiwa na matumaini ya kuendeleza rekodi ya kushinda nyumbani katika mechi zote msimu huu

United wanaingia katika mchezo huu wakiwa wametoka kushinda mchezo wa raundi ya 6 ya Carabao Cup vs Swansea City baada ya kufungwa na Huddersfield wikiendi iliyopita.

Tottenham Hotspur

Spurs wamekuwa na matokeo mazuri hivi karibuni, wameshinda mechi 4 mfululizo za ligi – wakiifunga Liverpool 4-1 katika uwanja wa Wembley Jumapili iliyopita wakiwa wametoka kupata sare ya 1-1 na Real Madrid pale Estadio Santiago Bernabeu katika Champions League. Vijana wa Pochettino walikuwa wamepoteza mchezo mmoja tu katika mechi 13 katika mashindano yote msimu huu kabla ya kufungwa na West Ham katika mashindano ya Carabao Cup lakini pamoja na hilo Spurs wamekuwa kwenye kiwango bora.

Hata hivyo kesho watakuwa wanamkosa mshambuliaji wao Harry Kane ambaye amepata majeruhi ya misuli ya paja. Kane anaongoza kwa ufungaji wa magoli EPL, akiwa na magoli 8, msimu uliopita Spurs walicheza mechi 8 za ligi bila Kane, wakishinda 5 na sare 3. Wakifunga magoli 13 katika mechi hizo.

Spurs pia wanaringia rekodi yao nzuri ya ulinzi katika ligi, wameruhusu magoli 6 tu katika ligi.

Taarifa za Vikosi vya Timu

Jose Mourinho amethibitisha baada ya mchezo wa Swansea kwamba Phil Jones yupo fiti kucheza vs Spurs baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Huddersfield, Eric Bailly amepona na Marcos Rojo ameanza mazoezi akijiandaa kurejea kikosini. Hata hivyo mpaka sasa hakuna taarifa za maendeleo ya afya za Paul Pogba, Michael Carrick na Marouane Fellaini, ingawa Pogba tayari ameonekana amerudi mazoezini.

Spurs kwa upande wao – Danny Rose na Mousa Dembele wamerejea kikosini, lakini Lamela na Victor Wanyama wataungana na Kane katika benchi.

Takwimu na Rekodi

Kihistoria United wana rekodi bora sana vs Spurs, wameshinda mechi 87 katika mechi 186 zilizopita katika mashindano yote, sare 48 na Spurs wameshinda 51. Katika mechi 50 zilizopita za Premier League – United wameshinda mechi 3. Spurs wameshinda 7 na sare 11. Timu hizi zilifungana msimu uliopita – kila timu ikishinda kiwanjani kwake

Clean sheet kings

Mchezo wa kesho unawakutanisha magolikipa ambao wana rekodi bora kuliko wote katika ligi msimu huu. David De Gea anaongoza kwa kuwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu wavu wake kuguswa, ameruhusu magoli 4 tu, magoli hayo katika mechi za ugenini dhidi ya Huddersfield na Stoke, wakati golikipa wa Spurs Hugo Lloris ana clean sheet 5 lakini mechi ya mwisho kucheza na United bila kuruhusu goli ilikuwa White Hart Lane mwaka 2014.

Vita ya Ufungaji bora

Lukaku alianza ligi vizuri na kufunga magoli 7 wakati Kabe alianza taratibu kwa kuwa na mwezi mkame wa August, September akawasha moto na mpaka sana anaongoza kwa kuwa na magoli 8 kwenye ligi. Lukaku alianza kwa kufunga magoli 11 katika mechi 11 za mashindano yote, lakini hajafunga goli katika mechi 4 zilizopita. Kane hatohusika na mchezo wa kesho. Msimu uliopita Kane alimzidi Lukaku kwa magoli na kutwaa kiatu cha dhahabu akifunga magoli 29, safari hii Lukaku anahitaji kulipiza na kesho itakuwa siku muafaka kurudisha fomu yake ya kufunga.

Mourinho vs Pochettino

Jose Mourinho anakutana na kocha ambaye amemfunga mara 9 katika mechi 12. Amepoteza mechi 2 na sare 1. Katika mechi hizo Mourinho na kikosi chake wamefunga magoli 29 na sare wameruhusu magoli 8.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here