Home Kimataifa Ona manahodha maarufu duniani walivyopiga kura zao, Cr7 na Messi wakwepana

Ona manahodha maarufu duniani walivyopiga kura zao, Cr7 na Messi wakwepana

9594
0
SHARE

Kura zimepigwa kumtafuta mshindi wa tuzo ya The Best Fifa, na manahodha walipewa nafasi kupiga kura kwa kuandika majina matatu matatu, wafuatao ni baadhi ya manahodha maarufu na jinsi walivyopiga kura.

Eden Hazard, Hazard hakuona sababu ya kumnyima nyota mwenzake wa Chelsea Ngolo Kante kura, huku kura ya pili akimpigia nyota wa Real Madrid Cr7 na kura ya tatu akimpigia Luca Modric.

Lioneil Messi, kwa upande wa Messi yeye kura yake ya kwanza alimpigia Luis Suarez na ya pili akampa kiungo wa Barcelona Andres Iniesta huku kura yake ya tatu na ya mwisho akimpigia nyota wa PSG Neymar.

Brazil kura yao ilipigwa na Dani Alves ambaye aliwaweka wachezaji wote watatu walioingia tatu bora akianza na Neymar kisha akampigia Lioneil Messi na kura yake ya tatu akampigia Cristiano Ronaldo.

James Rodriguez nahodha wa Colombia yeye hakumpigia kura Lioneil Messi alianza na Cr7 kisha akampigia Sergio Ramos na ya tatu akampigia Robert Lewandoski.

Gianluigi Buffon mlinda lango wa Italia naye hakumpigia kura Messi bali kura yake ya kwanza ilienda kwa Cr7 ya pili akampa Paulo Dyabala na ya tatu akampigia Luka Modric.

Obi John Mikel nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria yeye alianza na Lioneil Messi, ya pili akampigia Cristiano Ronaldo na ya tatu akampigia Gianluigi Buffon.

Sergio Ramos aliweka unazi pembeni lakini kama kawaida jina la Cr7 alianza nalo kisha likafuatia na Lioneil Messi na jina lake la tatu akampigia Luca Modric.

Cristiano Ronaldo yeye kwa upande wake aliwapigia wachezaji wenzake wa Real Madrid kura akianza Luka Modric jina la pili akaweka Sergio Ramos kisha akamaliza na Marcelo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here