Home Kitaifa Mlipili amecheza mechi ya kwanza VPL tangu asajiliwe Simba, hii ni comment...

Mlipili amecheza mechi ya kwanza VPL tangu asajiliwe Simba, hii ni comment ya Omog 

7482
0
SHARE

October 21, 2017 ni siku ya kukumbukwa kwa beki wa kati wa Simba Yusuph Mlipili ambaye amecheza mechi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara akiwa amevaa uzi wa Msimbazi wakati Simba ilipocheza dhidi ya Njombe Mji na kuisadia timu yake kushinda 4-0.

Mlipili alianza kwenye kikosi cha kwanza kwenye beki ya kati sambamba na mganda Juuko Murshid, wawili hao walikuwa wakicheza pamoja kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya ligi na kufanikiwa kucheza dakika 90 bila kuruhusu goli chini ya uongozi wa golikipa wao Aishi Manula.

Baada ya mechi kumalizika, kocha wa Simba amesikika akimtaja Mlipili kuwa ni beki bora wa baada wa Simba

“Mlipili ni miongoni mwa mabeki wa kati bora wa baadae wa timu hii, ni mchezaji mzuri alifanya vizuri kwenye mechi yetu ya kirafiki tuliyocheza Dodoma”-Joseph Omog.

Omog amesema kikosi chake kilikuwa na mabadiliko makubwa kwenye mchezo wa leo kwa sababu ana wachezaji wengi lakini baadhi ya wachezaji wake wanauguza majeraha.

Tangu kuanza kwa msimu huu Method Mwanjale, Salim Mbonde na Juuko Murshid wamekuwa wakibadilishana katika sehemu ya ulkinzi wa kati katika mechi zilizo pita kabla ya mchezo wa leo.

Mlipili alisajiliwa Simba akitokea Toto Africans timu iliyoshuka daraja msimu uliopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here