Home Kimataifa Ukame wa mabao waikumba Santiago Bernabeu, haijawahi tokea tangu 2003/2004

Ukame wa mabao waikumba Santiago Bernabeu, haijawahi tokea tangu 2003/2004

5041
0
SHARE

Tangu msimu wa ligi kuu nchini Hispania La Liga kuanza, mabingwa watetezi wa ligi hiyo Real Madrid wanaonekana kusuasua sana huku kukiwa na ukame mkubwa wa mabao tofauti na msimu uliopita.

Msimu uliopita uwanja wa Santiago Bernabeu ulionekana kama machinjio makuu ya wapinzani lakini msimu huu pana hali ya ukame mkubwa wa mabao ambao haujawahi tokea kwa misimu saba iliyopita.

Real Madrid wamecheza michezo 7 katika uwanja huo wa Santiago Bernabeu lakini mabao waliyopata katika michezo hiyo ni mabao 11 ambayo ni idadi ndogo ya mabao na mara ya mwisho hali hii ilitokea msimu wa 2003/2004.

Upungufu wa  mabao Madrid unaashiria nini? Iko wazi kwamba majeraha ya Gareth Bale yanaitesa Madrid huku adhabu aliyopewa Cr7 kukosa mechi kadhaa za msimu pia ni tatizo lakini iko wazi kwamba Madrid eneo lao la ushambuliaji haliko vizuri.

Haliko vizuri kwa sababu viungo Toni Kroos na Luca Modric wameshapiga pasi 108 kwenye nusu ya tatu ya wapinzani lakini idadi ya mabao iliyopo ni pungufu mnoo tofauti na pasi zinazopigwa kwenye lango la wapinzani.

Zinedine Zidane anaweza kubeba lawama kwa upande mwingine kwa kumruhusu Alvaro Morata na James Rodriguez waondoke wakati kikosi chake hakikuwa na uhakika wa washambuliaji waliopo kuwa vizuri.

Wastani wa ufungaji wa Real Madrid katika Champions League ni 14% ambayo ni ndogo zaidi katika michuano hiyo huku wakiwa wamezidiwa mabao 9 na vinara wa La Liga klabu ya Barcelona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here