Home Kimataifa Safu butu ya ushambuliaji ya Atletico Madrid itawagharimu msimu huu

Safu butu ya ushambuliaji ya Atletico Madrid itawagharimu msimu huu

5156
0
SHARE

Ufungaji wa wa magoli ni tatizo ambalo limedhihirika kuwa ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya Atletico Madrid msimu huu na matokeo yake timu imekuwa ikipoteza sana msimu huu wa 2017/18 kama ambavyo ilionekana juzi katika mchezo dhidi ya Qarabag kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya.

Baada ya michezo 11 msimu huu – mechi 8 kwenye La Liga na mechi 3 za Champions League – Atletico wamefunga magoli machache kuliko wakati wote ambao Simeone amekuwa kocha – wamefunga magoli 14 tu, magoli 5 kati ya hayo wameyafunga katika mchezo mmoja dhidi ya Las Palmas mwezi August.

Msimu uliopita, Atletico walikuwa wamefunga magoli 24 mpaka kufikia hatua kama hii ni Leganes tu ndio walifanikiwa kucheza nao bila nyavu zao kutikiswa na washambuliaji wa Simeone kwenye michezo 11 ya kwanza.

Msimu wa 2015/16 Antoine Griezmann akiwa na Jackson Martinez, Fernando Torres, Angel Corre na Luciano Vietto – Rojiblancos walikuwa wameshafunga magoli 18, 13 pekee yakifungwa na washambuliaji tu.

Msimu wa 2014/15, Griezmann akiwa na Mario Mandzukic katika ushambuliaji, walikiisaidia kikosi cha Simeone kufunga magoli 22 katika mechi 11 za mwanzo.

Falcao na Diego Costa waliongoza kwa kufunga magoli 25 kwenye mechi 11 za mwanzo msimu wa 2012/13, lakini msimu ambao Atletico Madrid walianza vizuri zaidi ulikuwa msimu wa 2013/14 ambapo walifunga magoli 26 kwenye idadi hiyo ya mechi – msimu huu walimaliza wakiwa mabingwa wa La Liga na wakafika fainali ya Championd League.

Atletico wanashika nafasi ya 4 kwenye ligi, kwenye kundi lao la Champions League wanashika nafasi 3 nyuma ya Chelsea na Roma. Wanahitaji kutafuta suluhisho kwenye safu yao ya ushambuliaji au wataishia kwenye Europa League na kuikosa top 3 ya La liga msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here