Home Kimataifa West Bromich Albion na laana ya kuwaachisha kazi makocha wa timu nyingine...

West Bromich Albion na laana ya kuwaachisha kazi makocha wa timu nyingine EPL, hata Ferguson walimsindikiza 

6682
0
SHARE

Hata haikuchukua zaidi ya masaa 24 kwa mabosi wa Leicester kumtimua Craig Shakespeare baada ya sare dhidi ya West Brom, na hii ulikuwa muendelezo wa West Brom kuwaachisha na kuwafukuzisha kazi makocha.

Rekodi zinaonesha katika ligi kuu Uingereza ukikutana na West Brom huku kocha akiwa katika presha kubwa baasi ujue upo uwezekano mkubwa sana afukuzwe akishindwa kuwafunga kama rekodi zinavyoonesha.

Andre Villas Boas,March mwaka 2012 Villas Boas hakuwa amefanya vizuri sana kwani alishinda mara mbili katika mechi 12, lakini alipokutana tu na West Bromich Albion walipomfunga bao moja siku hiyo hiyo Roman Abromovich akamfukuza AvB.

Roberto Di Matteo, sasa mwaka huo huo Chelsea wakawa na Roberto Di Matteo kocha ambaye aliwapa ubingwa wa Champions League, lakini Chelsea hawakuwa wanafanga vizuri sana na walipopigwa bao 2 kwa 1 na West Brom mwezi November 2012 Chelsea wakamtimua Di Matteo.

Roberto Mancini, tofauti na Di Matteo na Boas, huyu Mancini hakufungwa na West Brom bali walikuja pale Etihad wakala bao moja kiroho safi lakink mwenendo wa City haukuwaridhisha waarabu wa Man City baada ya ushindi huo wakamfukuza Mancini.

Paulo Di Canio, alitoka kushinda michezo 3 kati ya 13 katika Epl na mabosi waliendelea kumuamini na kumpa muda, walipoenda kuitembelea West Brom September 21 mwaka 2013 wakapigwa bao 3 kwa nunge na hapo hapo Sunderland wakamuondoa kikosini.

Chris Hughton, mwezi April mwaka 2014 Norwich walikuwa nyumbani kuwakaribisha West Bromich Albion na wakati huo Hughton alikuwa kwenye presha kubwa lakini alipopigwa tu bao 1 kwa nunge nyumbani ukawa mwisho wake kuifundisha Norwich.

Sir Alex Ferguson, May 19 2013 ni kati ya siku mashabiki wa United hawataki kuikumbuka kwa kuwa ndio siku SAF aliamua kustaafu, mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ga West Brom ambapo walitoka sare ya bao 5 kwa 5 na tangu hapo Fergie akaachana na ukocha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here