Home Kitaifa “Sijaja Simba kufanya maajabu”-Kocha mpya

“Sijaja Simba kufanya maajabu”-Kocha mpya

10677
0
SHARE

Kocha msaidizi mpya ndani ya kikosi cha Simba Masud Djuma amesema hajaenda klabuni hapo kufanya maajabu bali ni kutoa mchango wa kile alichonacho kwa kushirikiana na benchi la ufundi lililopo sasa.

“Sijaja kufanya maajabu, nimekuja kuisaidia Simba kwa kidogo nilichonacho ili kuisogeza mbele zaidi”-Masud Djuma kocha msaidizi Simba.

Kuhusu ukali

Unaambiwa Djuma huwa ni mtata kwa wachezaji hasa pale wanapokuwa kinyume na maelekezo yake.

Amesema yeye ni mtu wa pande mbili, mkali na mpole lakini huwa mkali pale ambapo mchezaji anataka kuharibu kazi.

“Mimi ni kama kiganja cha mkono, kina pande mbili. Mimi ni mpole lakini kwa upande mwingine ni mkali. Nimekuja hapa kufanya kazi ili kuipeleka Simba mbele na mimi nisogee mbele.”

Kuhusu kutoka kuwa kocha mkuu hadi kocha msaidizi Simba.

Alikuwa kocha mkuu msimu uliopita wakati anaifundisha Rayon Sport ya Rwanda kabla ya mkataba wake kumalizika. Akashinda tuzo ya kocha bora wa msimu wa Azam Rwandan Premier League.

“Nilianzia chini, baafa ya kuwa kocha bora Rwanda nikasema sitaki tena kuwa kocha msaidizi ndani ya Rwanda nimekuja hapa kuwa chini ya kocha mkubwa ni kama mzazi kwangu nahitaji kujifunza kutoka kwake ili nipande.”

Anaijua vizuri mechi ya Simba na Yanga

“Nimezaliwa nimekuwa nazisikia Simba na Yanga, kila sehemu kuna mechi zenye presha kubwa siwezi kuahidi lolote kuhusu mechi ya Simba na Yanga kwa sababu mpira una matokeo matatu.”

Kuhusu kutimuliwa

Amesema makocha ni sawa na mabegi, hayapaswi kufunguliwa zipu hadi mwisho kwa sababu muda wowote unaweza ukafunga zipu na kuondoka.

“Sisi makocha ni kama mabegi, hupaswi kufungua zipu yote kwa sababu muda wowote unaweza kuondoka.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here