Home Kitaifa Hivi unajua kama Okwi amefunga magoli mengi zaidi ya timu 12 za...

Hivi unajua kama Okwi amefunga magoli mengi zaidi ya timu 12 za VPL?

5264
0
SHARE

Mchezaji wa Simba Emanuel Okwi amefunga magoli saba (7) hadi sasa katika mechi tano za ligi alizocheza msimu huu, magoli mengi zaidi ya timu 12 kati ya 16 za VPL.

Amefunga magoli hayo (7) dhidi ya Ruvu Shooting (4), Mwadui (2) na Mtibwa Sugar (1), magoli yote ameyafunga kwenye uwanja wa Uhuru, Dar. Hajafunga katika mechi mbili Mbao 2-2 Simba na Stand United 1-2 Simba huku akikosa mchezo mmoja wa ligi Azam 0-0 Simba.

Okwi ndio anaongoza mbio za wafungaji wa VPL msimu huu akiwa amemwacha kwa magoli matatu mtu anaemfuatia ambae ni Mohamed Rashid ea Tanzania Prisons mwenye magoli manne.

Okwi amevizidi vilabu hivyo ambavyo vimecheza mechi sita lakini havijafikia magoli saba. Mtibwa Sugar (6), Yanga (6), Azam (5), Singida United (6)  Ndanda (4), Lipuli (3), Njombe (3), Mwadui (6), Ruvu Shooting (3), Majimaji (4), Stand United (3) na Kagera Sugar (2).

Timu tatu pekee ndio zimefunga magoli mengi zaidi ya Okwi, Simba (15), Tanzania Prisons (8) na Mbao. Mbeya City imefunga magoli saba (7) sawa na magoli yote ya Okwi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here