Home Kitaifa “Haijawahi kupita tar 2 Simba haijalipa mishahara”-Manara

“Haijawahi kupita tar 2 Simba haijalipa mishahara”-Manara

5383
0
SHARE

Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema klabu yao haijawahi kuzidisha zaidi ya tarehe mbili (baada ya mwezi kumalizika) kulipa mishahara ya wachezaji pamoja na benchi lake la ushindi.

Manara alikuwa akifafanua kuhusu kuhusu tuhuma za mitandao ya kijamii zilizoelekezwa kwa klabu ya Simba kwamba aliyekuwa kocha wao msaidizi Jackson Mayanja amekimbia njaa ndani ya klabu hiyo.

“Haijawahi kupita tarehe mbili Simba haijalipa mishahara wachezaji wala benchi la ufundi. Jana mlimsikia wenyewe kocha Mayanja”-Haji Manara.

“Omog bado ni kocha wa Simba hajaondoka kama baadhi ya mitandao ya kijamii ilivyoandika kwamba Omog ameandika barua ya kuomba kuondoka kwa sababu ya njaa.”

Jana Jumatano October 18, 2017 Mayanja alitangaza kujiuzulu nafasi yake ya ukocha msaidizi kwa sababu ya kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here