Home Kimataifa BBC iko hoi, MSN  tayari imekufa, MCN haoo wanauchukua mpira La Liga...

BBC iko hoi, MSN  tayari imekufa, MCN haoo wanauchukua mpira La Liga wanaupeleka Ligue 1

10936
0
SHARE

Upi utatu uliokuwa ukikugusa sana katika soka? Ni ule utatu ambao Bale anakimbia na mpira toka goli lao hadi la wapinzani na kuusukuma kwa Benzema kisha anatupiwa Ronaldo kuwamaliza wapinzani(BBC) na wanabeba Champions League?

Au ule utatu wa wahuni kutoka America Kusini ambapo Neymar anakusanya kijiji chote kinamfuata anamsukumia Suarez ambaye anawaangusha mabeki kabla ya kumsukumia Lioneil Messi La Pulga awaumize timu pinzani? (MSN)

Hao sio wa kwanza, unakumbuka utatu wa Carlos Tevez, Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo pale United? Je Pipo Inzaghi, Ricardo Kaka na Andrea Pirlo waliowaua Liverpool bao 2 kwa 1 pale Olympique Stadium 2007? 


Kila zama zina mwisho wake na ni wazi sasa zama za MSN zimekwisha, Neymar hayupo huku Suarez hayuko fiti amebaki Messi, BBC nako Bale majeraha kila kukicha, Benzema amekwisha huku Cristiano Ronaldo umri huooo unampa mkono na anafunga kwa kusua sua.

Ni muda wa MCN sasa kukiwasha, na kinachovutia kuhusa utatu huu ni kwamba unajengwa na vijana wadogo sana wakipata uzoefu kwa mkongwe mmoja huku kukiwa na mchanganyiko wa soka la Ulaya na America wote wakiwa na njaa ya kuiteka dunia.

Unapokuwa na mkusanya kijiji mwenye umri mdogo kama Mbappe mchezaji ambaye dunia kwa sasa inamzungumzia yeye na anataka kuonesha nini anacho, una Neymar anayepigiwa chapuo kubeba Ballon D’Or na Cavanni anayetaka kuonesha bado yupo yupo, unatarajia nini kama sio magoli tu?

Haishangazi hata kidogo kuona hadi sasa PSG weshaweka kambani mabao 43, ndio haishangazi na itashangazaje wakati katika kikosi chako una washambuliaji viwembe wa namna hii, kazi kubwa waliyonayo mashabiki wa PSG kwa sasa ni kuamka tu na kushangilia utatu huu.

Michezo sita MCN waliyocheza kwa pamoja wameweka kambani mabao 17, ikiwa ni wastani wa mabao matatu katika kila mchezo mmoja rekodi ambayo tayari imekuwa tishio kwa wapinzani wa PSG msimu huu na sio uongo wanatisha sana.

La kuvutia zaidi kuhusu MCN ni kwamba wote wanaonekana wana njaa sana ya kufunga na ndio sababu inayoleta ushindani wa kufunga katika timu yao, jambo ambalo linaongeza idadi ya mabao PSG.

Edison Cavanni ameshasema wao hawajaenda PSG kuwa marafiki, kwa maana nyingine hawajaenda PSG kuuza sura bali wameenda kupambana kwa ajili ya timu na wao kama wao MCN wako hapo kufunga tu na sio kingine.

Mabao 43 ambayo PSG wamefunga katika msimu huu, 58% yametoka kwa wanyama hawa na hii inamaanisha wachezaji wenhine wote wa PSG wamechangia 48% tu ya mabao ya PSG msimu huu, tuombe mungu atupe uhai lakini naamini MSN hawasimamishiki na watawasha moto zaidi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here