Home Kimataifa Baada ya kupotezwa uwanjani Romelu Lukaku aliamua kumpiga teke la usoni mlinzi...

Baada ya kupotezwa uwanjani Romelu Lukaku aliamua kumpiga teke la usoni mlinzi wa Liverpool

6802
0
SHARE

Mwishoni mwa wiki kulikuwa na mchezo mkubwa katika uwanja wa Anfiled ambapo wenyeji Liverpool waliikaribisha Manchester United katika dimba hilo mchezo ulioisha kwa suluhu.

Mchezo ambao United walionekana kuelemewa huku mshambuliaji wao Romelu Lukaku akionekana kupotezea kabida uwanjank na walinzi wa Liverpool waliokuwa wakiongozwa na Dejan Lovren.

Baada ya mchezo huo kuisha Lovren ametoa shutuma kali dhidi ya Lukaku na kudai kwamba mshambuliaji huyo alimpiga teke katika uso wake, tukio analosema halikuwa bahati mbaya na ilikusudiwa.

Lovren anasema wakati akijaribu kufanya tackling dhidi ya Lukaku aliona kiatu chake kikimpiga usoni na kwa jinsi alivyopigwa aligundua kwamba teke hilo lilikuwa la makusudi.

Dejan Lovren anasema kama Lukaku alichofanya ingekueawa ni bahati mbaya baasi angejaribu hata kuomba msamaha lakini baada ya mchezo huo mshambuliaji huyo alikaa kimya na hakusema chochote.

Alipoulizwa ni nini atafanya baada ya Lukaku kumfanyia tukio hilo, Lovren amesema hawezi kufanya lolote kwa kuwa jambo hilo limetokea ndani ya uwanja na yeye inabidi aliache hapo hapo uwanjani.

Taarifa zinasema chama cha soka nchini Uingereza FA wameona tukio hilo lilikuwa la bahati mbaya na hawana mpango wa kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here