Home Kimataifa Antonio Conte aandika rekodi mbovu nyingine wakati wakibanwa mbavu darajani, matokeo ya...

Antonio Conte aandika rekodi mbovu nyingine wakati wakibanwa mbavu darajani, matokeo ya CL Jumatano ya leo haya hapa

8690
0
SHARE

Eden Hazard alifunga mara mbili, idadi ambayo ni kubwa kuliko magoli yote aliyofunga katika mechi 14 za Chelsea zilizopita na David Luiz alifunga moja katika sare ya bao tatu tatu dhidi ya As Roma.

Mabao ya As Roma yeliwekwa kimiani na Aleksandre Kolarov na Eden Dzeko aliyefunga mara mbili na kumfanya Antonio Conte kwa mara ya kwanza kuruhusu mabao 3 katika mechi moja ya Champions League.

Lioneil Messi alifunga bao lake la 100 katika michuano ya soka Ulaya wakati Barcelona wakiifunga Olympiacos mabao 3 kwa 1 huku mabao mengine yakiwekwa kimiani na Nikolaou na Lucas Digne, huku Gerrad Pique akipewa kadi yake nyekundu ya kwanza katika Champions League.

Juventus walitoka nyuma ya bao moja na kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Sporting Cp huku mabao ya Juventus yakiwekwa kimiani na Stefanl Sturalo huku la ushindi likiwekwa kimiani na Mario Mandzukic.

Paris Saint German waliibuka kidedea kwa mabal 4 kwa nunge huku Kylian Mbappe, Edson Cavanni,Neymar na Di Maria wakifunga na goli la Cavanni likamfanya kuwa mchezaji wa 3 kufunga katika michezo 7 mfululizo katika Champions League baada ya Niestrooy na Cr7.

Matokeo mengine Manchester United waliichapa Benfica bao 1 kwa sifuri bao la Marcus Rashford, Bayern Munich wakawapiga Celtic 3 kwa nunge, Athletico Madrid na Quarabag Fk wakaenda sare ya bila kufungana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here