Home Kitaifa Ukweli kuhusu taarifa za Bakhresa kuweka ‘mzigo’ Simba

Ukweli kuhusu taarifa za Bakhresa kuweka ‘mzigo’ Simba

24931
0
SHARE

Kuna taarifa imeenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba tajiri Said Salim Bakhresa ameonesha nia ya kuwekeza ndani ya klabu ya Simba katika mchakato mpya wa kumtafuta mwekezaji baada ya klabu hiyo kubalidili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kutoka mfumo wa wanachama kwenda mfumo wa kampuni.

Inatajwa kuwa, Bakhresa anataka kuweka bilioni 25 kwa ajili ya kushindana na wawekezaji wengine kitu ambacho kimezua mijadala mbalimbali. Kuna baadhi ya wadau wanasema apewe Bakhresa kwa sababu ametoa fungu kubwa lakini wengine wanadai Mo aongeze pesa huku wengine wakitaka Mo apewe nafasi kubwa kwa sababu aliwahi kutoa bilioni moja kwa ajili ya kuisaidia timu.

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo ambaye ni Mwenyekiti wa kamati maalum ya kusimamia mchakato wa zabuni ili kumpata mwekezaji katika mfumo mpya wa umiliki wa Simba amekanusha taarifa na kutoa ufafanuzi namna mchakato huo unavyo kwenda.

“Katika mchakato huu hatumwangalii mtu na hao watu wanaosema fulani ametoa kiasi fulani huo ni uongo kwa sababu watu wa kujua ni sisi, hatujafika huko na waelewe mtu akianza kucheza rafu sasa hivi tuna adhabu zitakuja mbele ya safari. Kuna watu ambao wanaweza wakapoteza sifa kwa sababu ya kufanya mambo ambayo hayakubaliki kwenye mchakato”- Thomas Mihayo.

“Mchakato mzima tunaufata kisheria ukianza kuwaambia watu mimi naweka kiasi fulani ni kosa ambalo linakuondoa kwenye mchakato kwa hiyo nikuhakikishie kwa asilimia 100 sisi hatuna taarifa hizo, ya mitaani acha yasemwe huwezi kuwakataza watu kusema lakini kwetu sisi hatuna Bakhresa, Mo, tuna waombaji watakaoombaji watakaokuja.”

“Mpaka sasa hatuna maombi yoyote ambayo tumeyapata sisi wenyewe na wala hatujawauliza secretariat au kamati ambao ndio wanapokea, wala hatuwezi kuwauliza kwa sababu sio kazi yetu. Mambo tunayafanya kisheria na kwa utaratibu ambao unaeleweka.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here