Home Kimataifa Mechi 5 ambazo United walifurahia zaidi kuwapiga Liverpool hizi hapa, wewe unakumbuka...

Mechi 5 ambazo United walifurahia zaidi kuwapiga Liverpool hizi hapa, wewe unakumbuka ipi?

2506
0
SHARE

5.Man United 1 Livepool 0 mwaka 2006. Unaweza kuuona ushindi mdogo lakini kwa Ferguson ulikuwa mkubwa sana, mchezo ulikuwa mgumu na Liverpool hadi dakika ya 89 walionekana wanaweza kupata suluhu ugenini, lakin bao la dakika ya mwisho la mlinzi Rio Frrdinand liliamsha furaha kwa mashabiki wa United

4.Man United 4 Liverpool 0 mwaka 2003. Kati ya mechi ambayo United waliifurahia sana ni hii, Ruud Van Niestrooy aliwaua mara mbili huku Giggs na Solskjaer wakifunga moja moha na Liverpool wakimaliza 10 uwanjani baada ya Sami Hypia kupewa kadi nyekundu.

3.Liverpool 1 Man United 2 mwaka 2002. Hii ilikuwa Anfield bwana, alikuwa Diego Folran ambaye alikuwa katika kiwango cha hali ya juu sana siku hii akimtesa Jerzy Dudek na kuweka kamba mbili

2.Manchester United 3 Liverpool 2 mwaka  2010. Dimitir Berbatov akiwa katika kiwango alianza kuitungua Liverpool na kisha akafunga la pili kabla ya kukamilisha hat trick, utamua zaidi katika ushindi huu ulitokana na Steven Gerrard alipoweka kamba mbili ndani ya dakika 6 na kuwashtua United.

1.Fa Cup 1999 Manchester United 2 Liverpool 1. Liverpool walitangulia kwa bao la kuongoza la Michael Owen na wakaamini mchezo huo wangeshinda, lakini baadae mambo yalibadilika na Dwirght Yorke akaisawazishia United kabla ya Ole Gunner Solsjkaer akitokea benchi kuisawazishia United na kuifanya 1999 kuwa ya mafanikio makubwa kwa United.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here