Home Kimataifa Hiki ndicho kilichopelekea Pochettino kusema “Gurdiola hana nidhamu na anapenda kuwadharau wenzake” 

Hiki ndicho kilichopelekea Pochettino kusema “Gurdiola hana nidhamu na anapenda kuwadharau wenzake” 

8141
0
SHARE

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspur Maurcio Pochettino ameonekana kuchukizwa na maneno yaliyotolewa na Pep Gurdiola na kusema hadharani kwamba anahisi kukosewa heshima na kocha huyo.

Haya yamekuja baada ya Pe Gurdiola kuipa Tottenham Hotspur jina jipya la “Timu ya Harry Kane” kitendo ambacho Pochettino amekitafsiri kama muendelezo wa Pep Gurdiola kudharau watu wengine.

Pochettino amesema anamjua vyema Pep Gurdiola tangu kabla hajajiunga na Barcelona na anaamini katika uwezo wa kocha huyo lakini anafahama Pep hana nidhamu na amekuwa hivyo kwa watu wengi.

Pochettino amesema anashangazwa sana na kitendo cha kocha huyo kuwaita “Timu ya Kane” wakati yeye mafanikio yake makubwa alipokuwa Barcelona yaliletwa na Lioneil Messi lakini hakuna aliyewaita “Timu ya Lioneil”

Pochettino amesema mafanikio ya timu sio mtu mmoja na maneno kama aliyosema Gurdiola yanawakera watu wengi na wengi wanajisikia vibaya na kuchukulia maneno hayo kama ukosefu wa nidhamu.

Kocha huyo wa Tottenham amesema wakati wa mapumziko katikati ya wiki alikuwa kimya akiamini Pep atampigia simu kuomba msamaha lakini kocha huyo hakufanya hivyo lakini akisema hilo halijawaathiri wachezaji wameishia kucheka.

Harry Kane amekuwa na misimu mizuri sana siku za usoni huku msimu huu akiwa ameweka kambani magoli 15 katika michezo 10 na pia akifunga mabao 11 kati ya 16 ya Tottenham msimu huu hali inayowafanya wengi kuamini anaibeba Tottenham.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here