Home Kimataifa Antonio Valencia alitoka dampo kuziba pengo la Euro Mil 80

Antonio Valencia alitoka dampo kuziba pengo la Euro Mil 80

3553
0
SHARE

Na Privaldinho Abiud

Walio wengi tumezaliwa tukawakuta wazazi wakikesha juani na wengine hata wakiokota makopo ili tu tuweke kitu kinywani. Samahani kama umezaliwa Osterbay. Pia samahani kama hukupata bahati ya kuishi na wazazi. Antonio Valencia siku hizi anaonekana amejichubua usoni. Sawa tu. Si pesa zake bhana? Au kamkopa mtu?

Nyuma ya mafanikio ya mtu kuna mnyororo mrefu sana. Huenda Valencia hakuwahi kuwaza kuichezea hata lipuli ya huko kwao sembuse Man UTD. Huenda labda na wewe upo Kyela Mbeya na unasuburia Migomba yako kama mitatu ikomae upate ndizi ukauze Matolo kwa upate nauli ya kuja Dar. Kutoka Mbeya hadi Dar hazifiki Km 1000 nafahamu kuwa unawaza sana utafikaje, lini na wapi, pole ila usiogope. Nina uhakika licha ya kwamba tuliambiwa tukikaa mjini mpaka October sisi wanaume ila hizi kauli zisikutishe, nakusihi sana wewe mwaki nani sijui, lima mpunga kwa wingi ipo siku utamiliki ghala lako kule tunduma kama sio kumiliki mgodi Nzega au Arusha.

Kwanini usikate tamaa?

Ukizungumzia mji maarufu kwa madawa ya Kulevya kule nchini Ecuador huwezi kuacha kutaja Neuva Loja. Ni mji wenye ubabe na uchafu wa kila namna. Sasa Valencia alizaliwa kule (mbagala au Ungalimited za kule). Hakuwahi kufikiria kwamba ipo siku atatembea kilometa 8,926 mpaka jiji la Manchester. Yaani ni kama wewe uliyepo masasi unawaza kwenda kuchukua watoto wa kali kule Copa Cabana Brazil. Unaweza kuona ni ndoto?

Wakati fulana najiuliza sana kwenye Idadi ya watu wa mji wa Sucumbios inafikia 57,727 Je Mabosi wa Villarreal walimwonaje Valencia? Unaweza Kuta hata mimi kuna watu kutoka Uholanzi wananifuatilia bila mimi kujua eh?

Ndio maana nimekwambia haijalishi hata kama upo Ikwiriri amini ipo siku utakwenda Jijini Mwanza ukamiliki mjengo wako wa maana Kule Capri Point.

Jiulize

Viatu vya shule alivyonunuliwa Valencia na wazazi wake kwenye soko la kule Quito Pinchincha ndivyo alikuwa akivitumia kuchezea mpira kwenye kiwanja cha Carlos Vernaza ambacho mama yake alikuwa na glosari pembeni, leo yupo ulaya kwenye kiwanja chenye watu 70,000?
Mama yake alikuwa muuza Pombe za kienyeji sawa na Mama Priva tu aliyewahi kuuza mbege! Nadhani kazi yake Valencia ilikuwa kama sio kubeba ndoo za Pombe basi ni kusambaza oda.

Kumekuwa na Wimbi la vijana wengi wapo mtaani wanaokota makopo na kwenda kuyauza. Kwa akina Valencia Hili lilikuwa bonge la dili kule Quito  wakati yeye na baba yake walikuwa wakiyatafuta makopo hayo kwa udi na uvumba. Huenda walikuwa wakimzungumka mama kwa kwenda kuyauza makopo hayo wakati mama yao yeye alikuwa akiyahitaji kuuzia mbege yake.

Riziki ya mbwa ni miguu yake. Mapafu ya Valencia na jitihada zake ndio umaarufu wake kule Ulaya.  Licha ya mafanikio na umaarufu alio nayo kwa sasa sio mtu wa kujivuna. Jamaa muda wote uwanjani amechomekea, hana tatizo na mtu. Ana chenga yake moja tu.. ile paap paap kama anaruka fulani hivi. Hiyo hiyo inamfanya aibadilishe familia ya mzee Valencia kule Quito.

Ni mara chache sana kumuona Valencia akifunga goli akionesha ishara yoyote kama swaga au manjonjo. Haamini sana katika kamera. Anafahamu kamera sio maisha yake. Anajua kuwa kamera zinapaswa zimfuate yeye. Rivaldo alifukuzwa Barcelona kwa kumgomea mwalimu kucheza alipopangiwa, Valencia nina uhakika hata leo akiambiwa adake yeye fresh tu. Yeye ni kazi .

Hakuwahi kuchagua kazi, hii inamfanya leo awe beki wa kulia bora kabisa machon pangu kwa wakati wake. Tunaweza kuwataja akina Dan Alves, Na carvajal kama Mabeki wa kulia wazuri duniani lakini tusipomweka Valencia kwenye kundi hili kwa sasa nasi inabidi tuanze kuokota makopo.

Ni kwambie tu, Valencia alikuja mjini hamjui mtu yoyote yule, tena hata nauli ya gari alilipiwa na Carlos.

Cristiano Ronaldo alipoondoka Man utd, Valencia alisajiliwa kutoka Wigan kuziba pengo la Ronaldo. Alipoaanza kufananishwa na Ronaldo alikataa na mwisho aliomba abadilishwe namba 25. Valencia alimaanisha hivi usilewe sifa kwa kufananishwa na watu waliokuzidi ikiwa hujawafikia. alijua wazi kuwa amesajiliwa kuziba Pengo la Euro Million 86 sio Vingine. Umeajiriwa kufanya kazi kwenye ofisi za watu, fanya kilichokupeleka.

Kuna kitu kidogo unacho maishani kama Chenga Moja ya Valencia amini huo huo ndio mtaji wako. Unaweza ukatoka Dampo na ukawa Reginald Mengi

#Tumeelewana??

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here