Home Kimataifa Achana na Liverpool vs United, hii ni michezo 4 ambayo hupaswi kukosa...

Achana na Liverpool vs United, hii ni michezo 4 ambayo hupaswi kukosa wikiendi hii

3348
0
SHARE

Sahau kuhusu Liverpool watakapoikaribisha Manchester United pale Anfield, lakini hii inaweza kuwa wikiendi tamu zaidi katika ligi za barani Ulaya tangu kuanza kwa msimu huu wa 2017/2018.

1.Lyon vs Monaco, wenyeji Lyon wako katika nafasi ya 8 ya ligi na watawakaribisha Monaco walioko nafasi ya 2 katika Serie A, Lyon wamepoteza mchezo mmoja msimu huu sawa na Monaco lakini wamesuluhu mara 3 zaidi ya wapinzani wao.

2.Borussia Dortmund vs Rb Leizp, BvB wamekusanya alama 19 katika michezo 7 ya Bundesliga ikiwa na maana kwamba wameacha alama mbili tu, tangu msimu uanze mwaka huu hawajawahi kudondosha alama 3.

Lakini Rb Leizp wakiongozwa na mshambuliaji anayekuja kwa kasi duniani Timo Werner watajaribu kutafuta ushindi wa 3 mfululizo katika Bundesliga huku wakijiamini kutokana na matokeo mazuri msimu uliopita.

3.Roma vs Napoli, katika michezo 36 waliyocheza klabu ya As Roma wanaonekana wababe wa Napoli ambapo wameshinda michezo 18 kati ya 36 huku Napoli wakishinda michezo 9 na wametoka suluhu mara 9 na wikiendi hii Roma watakuwa Stadio Olimpico kujaribu kuendeleza utemi.

4.Atletico Madrid Vs Barcelona, Diego Simeone ana rekodi mbovu sana dhidi Barcelona ambapo katika michezo 21 amepata ushindi mara mbili tu na safari hii anawakaribisha Barcelona ambao msimu huu wanaonekana hawashikiki.

Barcelona wamekusanya alama zote 21 katika michezo yao 7 katika La Liga huku Atletico walioko nafasi ya 4 nao hawajapoteza mchezo hata mmoja lakini wamesuluhu mara 3 na kupata jumla ya alama 14.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here