Home Kimataifa Zinedine Zidane na Jose Mourinho kutunishiana misuli kwa nyota huyu wa dunia

Zinedine Zidane na Jose Mourinho kutunishiana misuli kwa nyota huyu wa dunia

13628
0
SHARE

Mafahali wawili wenye nguvu zaidi duniani kifedha Real Madrid na Manchester United wanaonekana wanaweza kuingia vitani katika dirisha lijalo la usajili ili kumnasa Harry Kane.

Walianza Real Madrid ambao tayri taarifa zilikuwa zinasema Kane ndilo jina lililoko kwenye nafasi ya kwanza katika list yao ya usajili ujao na walikuwa tayari kutoa kiasi Tottenham watakachohitaji.

Lakini taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema kocha Jose Mourinho humuambii kitu kuhusu Harry Kane na kwa muda mrefu amekuwa akihitaji saini yake lakini anaona huu ni wakati muafaka kumnunua.

Mourinho anataka kujaribu kuwachezesha Lukaku na Harry Kane kwa pamoja ili kuongeza makali katika kikosi cha United kinachopigana kurudisha heshima yake iliyokuwa imeanza kupotea barani Ulaya.

Lakini kumnunua Harry Kane haiwezi kuwa kitu rahisi sana kwa Manchester United na Real Madrid kwani Tottenham wanatajwa kuhitaji kiasi cha £175m kwa mtu yeyote ambaye atahitaji huduma ya Kane.

Tangu msimu huu kuanza Harry Kane ameweka kambani mabao 15 katika michezo 13 na tayari anaongelewa kama mshambuliaji anayetisha zaidi ulimwenguni kwa sasa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here