Home Ligi Wanne ‘out’ Yanga kuikabili Kagera Sugar Kaitaba

Wanne ‘out’ Yanga kuikabili Kagera Sugar Kaitaba

7915
0
SHARE

Leo Alhamisi October 12, 2017 kikosi cha Yanga kinasafiri kwa ndege kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mechi yao ya ligi kuu Tanzania bara siku ya Jumamosi October 14, 2017 dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Katika mchezo huo, Yanga itawakosa wachezaji wake Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao wanasumbuliwa na majeraha. Kwa mujibu wa afisa habari wa Yanga Dismas Ten, Ngoma hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Kagera Sugar lakini anaweza akatumika kwenye mchezo dhidi ya Stand United kwa hiyo atasafiri na timu kuelekea Kanda ya Ziwa.

Wachezaji wengine watakaokosena ni Ramadhani Kabwili na Said Musa ambao wapo kwenye timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ambayo ipo kambini ikiendelea na mazoezi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here