Home Kitaifa Timu 8 zilizofuzu robo fsinali Ndondo Cup Mwanza

Timu 8 zilizofuzu robo fsinali Ndondo Cup Mwanza

1544
0
SHARE

Hatua ya makundi ya michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup jijini Mwanza imemalizika jana na kupatikana timu 8 zilizoingia hatua ya robo fainali.

Kutoka kundi A timu ya Mnadani FC imeongoza kundi hilo ikiwa na alama 7 na Iseni FC ikimaliza nafasi ya 2 kwa kuwa na alama 5.

Kundi B lililokua na patashika timu ya Mabatini Star imeongoza kundi hilo kwa alama 6 sawa sawa na Nyegezi Terminal zikitofautiana magoli ya kufunga.

Kundi C wajanja wa Milongo timu ya Milo Clyne imeongoza kundi hilo kwa kuwa na alama 9 huku nafasi ya pili ikishikwa na Morning Star wakiwa na alama 4 sawa na Power lakini Power wakiwa na idadi ndogo ya magoli.

Kundi D Phanton FC wamekuwa vinara kwa kuwa na alama 9 wakifuatiwa na AFC Lumumba waliokusanya alama 6.

Michezo ya hatua ya robo fainal inatarajiwa kuanza tarehe 16 October, 2017 siku ya Jumatatu uwanja wa Nyamagana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here