Home Kimataifa Raisi wa PSG aingia katika kesi kubwa ya kutoa rushwa

Raisi wa PSG aingia katika kesi kubwa ya kutoa rushwa

6153
0
SHARE

Taifa la Qatar bado linaandamwa na kesi ya rushwa, Qatar wabadaiwa kwamba walitoa rushwa ili wapewe nafasi ya kuandaa michuano ya soka ya kombe la dunia mwaka 2022 suala ambalo liliwaandama sana.

Nasser Al Khelaifi tajiri wa Qatar ambaye ndiye raisi wa klabu ya PSG naye ameingia katika kesi ya rushwa ambapo inadaiwa alitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa moja wa maafisa wa FIFA ili kupewa haki za matangazo.

Al Khelaifi ambaye majuzi tu aliishangaza dunia kwa kufanya usajili uliovunja rekodi ya dunia kumnunua Neymar anadaiwa kwamba alihitaji kumiliki haki za kurusha matangazo ya michezo ya kombe la dunia mwaka 2026 na 2030.

Jerome Vackle aliyekuwa secretary wa zamani wa chama cha soka duniani FIFA anadaiwa alipewa kiasi cha pesa kwa ajili ya kulisaidia shirika la Bein Sports kupata haki za matangazo hayo ya kombe la dunia.

Kuhusishwa kwa Al Khelaifi na kesi hii kunazidi kuiweka Qatar karibu skendo ya rushwa katika fainali za kombe la dunia 2022 ambapo kesi ya Vackle naye ambaye alitimuliwa na FIFA kutokana na kesi za rushwa anazidi kuchafuka.

Maofisa wa masuala ya rushwa kutoka Uswisi wamesema El Khelaifi ambaye ni bosi wa shirika la Bein Sports alilitumia shirika lake kama njia ya kupata tenda hiyo ya matangazo ya kombe la dunia na tayari maofisa hao wameanza uchunguzi dhidi ya Al Khelaifi.

Bado hadi sasa raisi huyo wa PSG hajazungumza lolote juu ya madai dhidi yake japo hii inaweza kuwa kesi kubwa itakayomchafua yeye pamoja na Qatar kuelekea fainali za kombe la dunia mwaka 2022.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here