Home Kitaifa Manne makubwa ya kuvutia Mbao vs Mbeya City CCM Kirumba

Manne makubwa ya kuvutia Mbao vs Mbeya City CCM Kirumba

4027
0
SHARE

Ligi kuu Tanzania bara itaendelea mwishoni mwa juma hili ambapo mechi zitachezwa kuanzia Ijumaa October 13 hadi Jumapili October 15, 2017. Kesho Ijumaa kutakuwa na mchezo mmoja kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kati ya wenyeji Mbao FC dhidi ya timu ya ‘kizazi kipya’ Mbeya City kutoka jijini Mbeya.

Vita ya warundi

Mbeya City wamemwajiri kocha  Nsanzurwimo Ramadhani kuwa kocha wao mkuu kwa mkataba wa msimu mmoja, kocha huyu ni raia wa Bundi kama ilivyo kwa kocha wa Mbao FC Ettiene Ndayiragije. Ndayiragije tayari ameonesha ubora wake kwenye ligi ya Tanzania hakuna mtu mwenye shaka na uwezo wake wa kiufundi tangu alipoanza kuifundisha Mbao.

Ndayiragije amefanikiwa kuiongoza Mbao kucheza fainali ya Azam Federation Cup ndani ya msimu wake mmoja, ameonesha ushindani dhidi ya vilabu vikubwa vya nchi hii kwa kuichapa Yanga mara mbili huku Simba wakipata wakati mgumu kupata matokeo dhidi ya timu hiyo na mara ya mwisho kukutana Simba waliambulia sare ugenini.

Tayari amepata uzoefu kwenye ligi ya Bongo licha ya kikosi chake kubomolewa na vilabu vyenye nguvu kiuchumi na majina makubwa lakini bado Mbao ni tishio kwenye ligi kutokana na uwepo wa kocha huyo.

Nsanzurwimo amekuja tayari ligi ikiwa imeanza, hajafanya maandalizi ya kutosha na timu kabla ya msimu, hii inaweza kumpa wakati mgumu kuingiza mbinu zake mpya kwenye kikosi ambacho tayari kimecheza mechi kadhaa za ligi chini ya walimu wengine. Atahitaji muda ili kuendana na kasi ya VPL lakini wakati yeye akihitaji muda, ligi inaendelea na huenda akaanza kukaribishwa na Mbao.

Mbao inahitaji ushindi wa kwanza nyumbani

Mbao imeshacheza mechi tano msimu huu sawa na timu nyingie zote za ligi, michezo  mitatu ya kwanza mfululizo ilicheza viwanja vya ugenini ikashinda mechi moja na kupoteza mingine miwili, ikarejea uwanja wake wa nyumbani CCM Kirumba na kucheza mechi mbili mfululizo ambapo ilitoka sare kwenye michezo hiyo.

Bado haijapata ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani (Simba 2-2 Mbao na Mbao 1-1 Tanzania Prisons), mchezo dhidi ya Mbeya City utakuwa ni wa tatu mfululizo kwa Mbao ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, kwa namna yoyote watakuwa wakihitaji matokeo ya ushindi kabla hawajaanza kutoka kwenda ugenini.

Mbeya City wanaweza wakawa wahanga CCM Kirumba wakati Mbao ikihitaji ushindi wa kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani CCM Kirumba.

Matokeo yaliyopita

Mbao imeshinda mechi moja tu kati ya mechi tano tangu kuanza kwa ligi msimu huu, imepoteza mechi mbili na kutoka sare katika michezo miwili, ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tano, pointi mbili nyuma ya Mbeya City yenye pointi saba.

 • Kagera Sugar 0-1 Mbao
 • Singida United 2-1 Mbao
 • Mtibwa Sugar 2-1 Mbao
 • Mbao 2-2 Simba
 • Mbao 1-1 Tanzania Prisons
 • Mbao ?? Mbeya City

Mbeya City imeshinda mechi mbili, imepoteza mbili na kutoka sare mchezo mmoja kati ya michezo mitano iliyopita ya ligi msimu huu, City bado haijashinda ugenini, mechi mbili ilizopata matokeo ya ushindi ni kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya. Ipo nafasi ya saba kwenye msimamo ikiwa na pointi zake saba.

 • Mbeya City 1-0 Majimaji
 • Mbeya City 0-1 Ndanda
 • Mbeya City 1-0 Njombe Mji
 • Stand United 2-1 Mbeya City
 • Mwadui 2-2 Mbeya City
 • Mbao ?? Mbeya City

Msimu uliopita unaibeba Mbeya City

Msimu uliopita Mbao ndio ilianza kucheza VPL kwa mara ya kwanza wakati Mbeya City ilikuwa inacheza kwa mara ya nne mfululizo, timu hizo zilipokutana Mbeya City ilishinda mechi zaote kwa kutoa vipigo vya nguvu nyumbani na ugenini.

Matokeo ya msimu uliopita yanaibeba Mbeya City dhidi ya Mbao kwa sababu walishinda mechi zote katika msimu huo.

 • Mbeya City 3-1 Mbao
 • Mbao 1-4 Mbeya City

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here