Home Kimataifa Lukaku anaweza kuweka rekodi hii? Koeman atatimuliwa? Haya ni baadhi ya maswali...

Lukaku anaweza kuweka rekodi hii? Koeman atatimuliwa? Haya ni baadhi ya maswali ya kujiuliza kuelekea weekend ya Epl

3168
0
SHARE

Michezo ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa wiki hii imemalizika na sasa tunakwenda katika ligi za vilabu, na kati ya wiki tamu katika soka ni wiki hii kwani mitanange mingi itakuwa moto moto.

Klopp atafanyaje dhidi ya United? Liverpool watakipiga dhidi ya Manchester United,mchezo huu unaweza kuwa na presha kubwa kwa Jurgen Klopp kutokana na matokeo anayoyapata siku za karibuni huku mshambuliaji muhimu Sadio Mane akiwa majeruhi.

Eneo la ulinzi haliko vizuri na Klopp analijua hilo,tusubiri kuona kama amelifanyia kazi eneo hilo au ataendelea kudoda mbele ya United wanaoonekana kuwa na washambuliaji viwembe.

Romelu Lukaku kuwa mchezaji wa kwanza kuweka rekodi hii? Tayari amefunga katika michezo 7 mfululizo ya Epl na huu ni mchezo wake wa 8 na kama akifunga atakuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michezo yake 8 ya mwanzo na timu mpya Epl.

United watachezaje bila Pogba na Fellaini? Baada ya Paul Pogba kupata majeraha kocha wa Manchester United alianza kumuamini Marouane Fellaini na sasa Fellaini naye ameumia huku hofu ya majeraha ikianza kuwatesa, Ander Herrera huenda akapewa nafasi na watu wanasubiri kuona nini atafanya.

Tottenham watapata alama 3 kwa mara ya kwanza Wembley? Wembley uwanja wa nyumbani wa Tottenham utawakaribisha Bournemouth, lakini Wembely pamekuwa pagumu mno kwa Tottenham na hawajawahi kupata alama 3 msimu huu na wiki hii wanatari labda wanaweza kuzipata.

Etihad kuendelea kuwa mahala pa kukatili wapinzani? Stoke City anakanyaga Etihad huku wageni wawili waliopita hapa walikula bao tano tano kila mmoja, Stoke wanaenda wakiwa wanayumba yumba nao wanaweza kupata walichopata waliotangulia.

Arsenal wataendeleza vipigo? Michezo minne iliyopita ya Arsenal wanaonekana kuanza kukaa vizuri, Jumamosi hii wataifuata Watford huku Alexis Sanchez akitoka kwenye majonzi ya kulikosa kombe la dunia lakini pia tunasubiri kuona kama Wenger atampa nafasi Wilshaire anayeonekana kutoswa Arsenal.

Brighton watamfukuzisha kazi Ronald Koeman? Ndio/Hapana hili linaweza kutokea, Everton wanaweza kuwa wamechoshwa na matokeo wanayopata ukizingatia kwamba walitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanya usajili lakini pia wanaweza kuendelea kumpa muda Koeman aijenge timu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here