Home Kimataifa Nani kama Messi? Apiga hat-trick, aweka rekodi,aibeba Argentina Sanchez akiondolewa

Nani kama Messi? Apiga hat-trick, aweka rekodi,aibeba Argentina Sanchez akiondolewa

14820
0
SHARE

Achilia mbali Argentina kuwa katika presha kubwa alfajiri ya leo lakini hakuna mchezaji ambaye alikuwa katika presha kubwa kama Lioneil Messi.

Wengi walishakata tamaa na wengi waliamini Messi ana nafasi ndogo kushiriki kombe la dunia mwakani lakini alichofanya alfajiri ya leo kinathibitisha kwamba yeye ni Lioneil Messi.

Lioneil Messi amewabeba Argentina katika mabega yake na kuwapeleka kombe la dunia baada ya kufunga hat trick katika ushindi wa bao 3 kwa 1 dhidi ya Ecuador.

Mabao ya Lioneil Messi yamemuweka kwenye vitabu vya rekodi vya Conimobel ambapo anakuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 21 wakati wa michezo ya kufudhu kwenye ukanda huo.

Ushindi wa Argentina unakuja huku Colombia na Peru wakitoka sare ya bao moja kwa moja na kuwafanya Argentina kumaliza nafasi ya 3, James Rodriguez aliifungia Colombia kabla ya Paulo Guererro kusawazisha.

Chile ambao hadi jana walikuwa nafasi nzuri walipigwa bao 3 kwa 0 na Brazil na kupelekwa hadi nafasi ya 6 itakayowalazimu kukosa kombe la dunia huku mabao ya Brazil yakifungwa na Paulinho na Gabriel Jesus (2).

Uruguay wamekaa katika nafasi ya pili baada ya kuikung’uta Bolivia 4 kwa 2 huku Luis Suarez akifunga mara mbili, Cavanni (1) na Martin Caceres 1.

Kwa matokeo haya sasa timu za taifa za Brazil, Uruguay,Argentina na Colombia zimefudhu moja kwa moja kombe la dunia mwakani huku Peru watalazimika kucheza kwanza mechi za mtoano.

Concacaf nako ndoto za USA kushiriki fainali za kombe la dunia zilizimwa baada ya Trinidad and Tobago kuwapiga bao 2 kwa mabao ya Alvin Jones na la kujifunga la Omar Gonzalez huku bao la USA likifungwa na Christina Pulisic.

Vinara wa kundi Mexico walipigwa bao 3 kwa 2 na Hondurus lakini haijuwatoa kileleni huku Hondurus wenyewe wakimaliza nafasi ya nne itakayowalazimu kucheza mtoano dhidi ya Australia.

Panama waliifunga Costa Rica bao 2 kwa 1 kupitia kwa Gabriel Torres na Roman Torres huku bal la Costa Rica likiwekwa kimiani na Johan Venegas lakini timu zote hizo zina tiketi ya kombe la dunia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here