Home Kimataifa Maskini Diego Costa, kocha Simeone aamua kumtosa

Maskini Diego Costa, kocha Simeone aamua kumtosa

5375
0
SHARE

Maisha ya Diego Costa siku za hivi karibuni yamekuwa sik ya kueleweka, tangu mtafaruku wake na kocha wake wa zamani Antonio Conte mshambuliaji huyo amekuwa haeleweki na haonekank uwanjani.

Lakini habari ambayo ilimfurahisha Diego Costa na kutuliza akili yake ilikuwa ni habari ya usajili wake kwenda Athletico Madrid kukamilika kwani Athletico ndipo mahali Costa alikuwa akipahitaji.

Lakini tayari maisha ndani ya Athletico Madrid yameshaanza kuwa machungu kwa Diego Costa baada ya kocha wa Athletico Madrid Diego Simeone kuamua kumtosa mchezaji huyo kupasha na kikosi cha kwanza.

Mwanzoni wakati Diego Costa anajiunga na Athletico alikuwa akichukua mazoezi na kikosi cha kwanza,baadaye kocha wa klabu hiyo alimuomba Costa kupasha na timu ya vijana jambo ambalo inadaiwa hajalifurahia.

Inasemekana Costa pamoja na kutopenda jambo hilo lakini baadae aliamua kukubali na kwenda katika kikosi cha vijana ambako hadi sasa ndio ambao anachukua nao mazoezi akisubiria mwezi January kuanza kucheza.

Kabla ya kuondoka Athletico Madrid mshambuliaji huyu wa Hispania aliichezea klabu hiyo jumla ya michezo 135 ambapo kati ya michezo hiyo alifanikiwa kufunga idadi ya mabao 64.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here