Home Kimataifa Je wajua yupo daktari wa meno aliyeipeleka timu Urusi 2018? Zijue timu...

Je wajua yupo daktari wa meno aliyeipeleka timu Urusi 2018? Zijue timu 10 toka Ulaya zilizofuzu kombe la dunia

6090
0
SHARE

1.Urusi. Hawa wana tiketi ya moja kwa moja kutokana na kuwa waandaaji wa michuano hii na hii itakuwa ni mara ya nne kwa taifa hili kushiriki kombe la dunia.

Urusi hawana majina makubwa katika timu yao, wachezaji wote walioichezea timu hii katika michuano ya confederation wanacheza ligi za ndani ya Urusi.

2.Uingereza. Wakiwa na kikosi kilichosheheni wachezaji wa Epl, wanakwenda wakiwa na kumbukumbu ya kufanya vyema mwaka 1966 na tangu hapo walifika nusu fainali ya michuano hii mara moja mwaka 1990.

Harry Kane yupo katika kiwango kinachoogopesha mabeki na Waingereza wote wanamuangalia mshambuliaji huyu kama silaha yao kubwa kufanya vyema kombe la dunia kocha Gareth Southgate anaangaliwa nini anaweza kuwapa Waingereza.

3.Ubelgiji, mwaka 2014 walitolewa katika robo fainali ya michuano hii nchini Brazil, lakini mwaka 1986 ndio walipata mafanikio makubwa wakimaliza nafasi ya 4.

Kutokana na kikosi chao kilichosheheni masupastaa kama Eden Hazard, Romelu Lukaku na Kelvin De Bruyne huku wakiwa na kicha mjuzi Robert Martinez wanatabiriwa kuwasha moto katika michuano hii.

4.Ufaransa, wanakwenda katika michuano hii wakiwa na kumbukumbu ya mwaka 1998 kuandaa michuano hii, mafanikio makubwa ya mwisho ilikuwa 2014 walipofika robo fainali lakini tofauti na siku za nyuma, safari hii wakiongozaa na kocha Didier Dechamps wanaingia na kikosi chenye vijana wadogo ila hatari.

Ufaransa ni kati ya timu ambazo hata mimi naamini watawasha moto mkubwa komba la dunia, Antoine Griezman, Paul Pogba na Kylian Mbappe wote ni wachezaji wenye umri mdogo na watakuwepo kuiongoza Ufaransa.

5.Iceland, kinatajwa kama kizazi cha dhahabu kuwahi kutokea Iceland, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki kombe la dunia na wanaamini watafanya makubwa.

Gylfi Siggurdson ndio mchezaji wao maarufu na atakuwepo mstari wa mbele kukiongoza kikosi hichi kinachonolewa na kocha Heimir Hallgrimsson ambaye kitaaluma ni dakatari wa meno lakini soka ilikuja tu kama kitu cha ziada.

6.Poland, mwaka 1974 na 1982 walumaliza katika nafasi ya 3 kombe la dunia, safari hii ni kati ya timu za kuongelewa sana huku wakiwa nafasi ya 6 viwango vya dunia.

Wanakwenda kombe la dunia huku wakiwa na mmoja wa wapasia nyavu waliokububu siku za usoni Robert Lewandoski akipasia nyavu mara 16 katika mechi za kufuzu.

7.Serbia, wataongozea na kiungo wa Manchester United Nemanja Matic lakini hawa sio wageni wa kombe la dunia kwani wameshashiriki michuano hii mara 11.

Branislav Ivanovic ambaye aliwahi kukipiga katika klabu ya Chelsea atakuwepo katika kikosi hiki kama mchezaji mkongwe akiwapa motisha vijana kubeba ndoo.

8.Hispania. Mwaka 2010 walitwaa kombe la dunia lakini Hispania wamekuwa wakikaa kileleni mwa viwango vya soka vya dunia kuanzia mwaka 2008, huwezi kutaja vikosi vya kuogopwa ukaacha hiki.

Historia na rekodi zinaweza kuwabeba Hispania lakini kiuhalisia safari hii inaonekana kuna mataifa tishio zaidi yao, Sergio Ramos, David De Gea na Alvaro Morata ni kati ya majina makubwa yatakayowabeba vijana wa Jullen Lopetegui.

9.Ureno. Mwaka 1966 ndio walipata mafanikio makubwa baada ya kumaliza michuano ya kombe la dunia katika nafasi ya 3, Cr7 atajaribu kupata kombe kubwa ambalo hana na hii inawafanya Ureno kuwa na morali.

Kocha Fernando Santos anafikiria kufanya kile wengi ambacho hawakutaraji alipobeba kombe la Euro na sasa anataka kufanya jambo hilo katika kombe la dunia

10.Ujerumani. Timu tishio sana kombe la dunia, kwanza ndio mabingwa watetezi lakini hii ndio timu bora duniani kwa sasa kutokana na viwango vya FIFA.

Wana uwiano mzuri kati ya vijana na wakongwe Antonio Rudiger,Leroy Sane na Thomas Muller ni baadhi ya majina ambayo kocha Joachim Low anaamini wanaweza kumpa kombe lingine la dunia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here