Home Kitaifa Hospitali waliolazwa Tukuyu ndiyo hiyohiyo watakayofia Jacaranda

Hospitali waliolazwa Tukuyu ndiyo hiyohiyo watakayofia Jacaranda

2522
0
SHARE

Na Privaldinho Abiud

Watu wangu wa MBEYA ugwe gu wandu wangu? Sijui nimepatia ama lah. Kila mtu Mbeya ni BIG hata kama una mwili kama wa kwangu unaitwa BIG.

Tuachane na hayo, miaka kama 31 imepita tokea Tukuyu Star wakiwa na wazee wetu kama Mzee Kanza Mrisho, Raphael Mapunda na Mohamed Kassanda walipotwaa Ubingwa wa Ligi kuu Bara. Kisha mwaka uliofuata klabu ya Tukuyu Star ilishuka daraja kwa kuwapoteza nyota wao maarufu kwa klabu za Simba na Yanga.

Mbeya City ya akina Matogolo, Mapunda, Mwigane Yeya, Kaseke na Mazanda wote hawa wameshatimka Mbeya City ni Mwasapili tu amebakia. Kizazi chao kipya kimezama kama ndoto za akina Spark na Zed Anto.

Wachezaji waliondoka Tukuyu walipukutisha kizazi chao kama barakutu na muziki wa bendi ulivyoburuzwa na kidalipo ya Mr nice. Mbeya City iliyokuwa ikasafiri na mashabiki wao waliocha kuuza ndizi soko la Mwanjelwa ili kuishabikia timu yao iko wapi? Kwishney.

Tukuyu Star ni zao la Mwenge Sport na Jamhuri Sport, ziliuzunganishwa na bwana Joseph Kasyupa Na Abdul Lausi hawakujua kama Tukuyu ingekuja kutambulisha vipaji murua kutoka Rungwe. Uongozi mbovu ulishindwa kuendeleza mawazo ya akina Kasyupa.

Mbeya City ilikuja kurudisha heshima iliyojengwa na Tukuyu miaka ya 1986 ndani ya uwanja wa Sokoine. Tukuyu Star ilimfanya mfanyabiashara maarufu kutoka Mbeya wakati ule Mzee Ramnik Pater Kaka awekeze katika klabu hiyo.

Vijana hawa wanaojiita Jacaranda Worriors wanatumia uwanja wa Sokoine nadhan unabeba mashabiki kama 20,000 hivi. Uwanja uleule waliozaliwaTukuyu na ni uwanja uleule waliofia tukuyu na ndio huohuo 2011 Mbeya City waliozaliwa na ndio huohuo umegeuka ICU na muda sio mrefu kama mgonjwa ataendelea kutafuniwa maji nae atafia hapohapo.

Mbeya City miaka minne makocha wanne, hali sio hali. 

Mbeya City inapaswa iwe miamba imara itakayowakilisha kusini miaka 20 ijayo ili kujenga njia kwa timu zingine. Walileta changamoto kwa timu kubwa sana za DSM lakini sijui kilichowakuta. Nina iman ile spirit ya akina ‘Mwakimbeyacity’ ikirudi tena basi kutakuwa na mgawanyiko mzuri wa kiushindani hapa TZ. Mtibwa Sugar kanda ya kati, kusini Mbeya City, ndugu zangu wa Mwadui nao wakikaza wawakilishe akina hayati Pamba na Kahama United, Kaskazini tushawachoka nyie endeleeni biashara na utalii tu mpira hamuuwezi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here