Home Kimataifa Netflix waingia mkataba na Juventus utakaowaumiza Manchester United na Barcelona

Netflix waingia mkataba na Juventus utakaowaumiza Manchester United na Barcelona

9556
0
SHARE

Kampuni inayohusu masuala ya kustream movie online ya Netflix imeingia ubia na klabu bingwa ya nchini Italia klabu ya Juventus na sasa wanakuja na jambo bora kwa ajili ya mashabiki wa soka watumiaji wa mtandao huo.

Netflix wameamua kutengeneza video ihusuyo maisha ndani ya wababe hao wa Italia (Documentary) ambapo ndani ya Documentary hiyo watazamaji watapata kuona karibia kila kitu ndani ya klabu hiyo.

Documentary hiyo itaonesha mechi za Juventus lakini pia itakuwa inaonesha matukio mbali mbali yanayotokea wakati Juventus wakiwa mazoezini, wakiwa vyumba vya kubadilishia nguo na wakiwa safarini.

Makamu mwenyekiti wa Juventus Federico Palomba amejinadi kwamba kwao hayo ni mafanikio makubwa sana na wao kama Juventus wanajisikia faraja kubwa kuwa klabu kubwa ya kwanza duniani kufanya hivyo.

Naye makamu wa raisi wa Juventus Erick Barmack anaamini klabu kama Juventus ina historia kubwa ambayo dunia inapaswa kuifahamu na kupitia Netflix itakuwa rahisi kwa ulimwengu kuijua Juventus.

Wakati Juventus wakiingia mkataba na Netflix inaonekana wazi itakuwa ngumu sana kwa sasa kumruhusu Paulo Dyabala kuondoka, hii inatokana na sababu kwamba ili documentary iangaliwe zaidi ni lazima kuwepo kwa wachezaji wakubwa.

Kulikuwa na tetesi kwa Paulo Dyabala kuihama klabu hiyo na kutimkia Barcelona au Manchester United lakini sasa ni inaonekana itakuwa ni ngumu zaidi kwa Juventus kumuacha aondoke kwani wanamuhutaji sio tu uwanjani bali na kuitangaza klabu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here