Home Kitaifa Athumani Machupa ametaja ‘top four’ yake ya VPL msimu huu

Athumani Machupa ametaja ‘top four’ yake ya VPL msimu huu

10336
0
SHARE

Mshambuliaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ametaja timu anazodhani zitamaliza katika nafasi za nne za juu (top four) baada ya kumalizika kwa msimu huu (2017/2018) ligi kuu Tanzania bara.

“Simba, Yanga, Singida United na Azam” ni ambazo amezitaja Machupa akiamini zitafanya vizuri ndani ya msimu huu kwa kuzingatia maandalizi pamoaja na usajili uliofanywa na vilabu hivyo vinne.

“Ukiangalia mwenendo wa ligi mpaka sasa hivi inaonesha timu zimejiandaa vizuri nah ii inatoa picha nzuri kama timu zinajiandaa vizuri tunaweza tukaona viwango vizuri zaidi na nimestushwa kuwaona Singida wako pale kutokana na uzoefu tulionao kuhusu timu zinazopanda kucheza ligi kuu.”

“Naona kuna mabadiliko na niseme ningependa ili tupandishe kiwango cheztu basi inabidi timu zizidishe maandalizi kwa zile ambazo hazijafanya maandalizi vizuri.”

“Kwa kawaida Tanzania tumezoea kuona Yanga, Simba na Mtibwa ndio zinapambania ubingwa lkakini mwaka huu inatupa sura kwamba kuna timu nyingi zinaweza kuwania taji la ligi kama Singida, Mtibwa, Yanga na Simba.”

“Watu wasiibeze Yanga na kuiondoa kwenye nafasi ya kuwania ubingwa kwa sababu bado wapo kwenye nafasi nzuri lakini Simba wamesajili vizuri ambnao hadi sasa wanaongoza ligi kitu ambacho kitawapa kujiamni kwa sababu wame-miss ubingwa kwa muda mrefu, kuongoza kwao ligi kutawaweka kuwa tayari kwa kila mchezo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here