Home Kitaifa “Kila  mechi kwetu ni fainali”-Alliance

“Kila  mechi kwetu ni fainali”-Alliance

1547
0
SHARE

Na Yohani Gwangway

Kocha mkuu wa timu ya Alliance Schools ya Mwanza Mbwana Makata amesema kila mchezo wa ligi daraja la kwanza kwao ni fainali baada ya ushndi wao wa magoli 3-0 mbele ya Biashara kutoka kule mkoani Mara uliorindima jana katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza

Mara baada ya mchezo Makata alisema vijana wake wa Alliance wamesikiliza mawaidha yake kuwa wanatakiwa kucheza mchezo huo kwa nguvu na kuuchukulia kila mchezo kama fainali kutokana na kuhitaji kupanda ligi kuu ya Vodacom msimu ujao

Mbwana Makata alipozungumzia wapinzani wake, alisema timu ya Biashara iliiga mchezo wao hivyo kujikuta katika wakati mguu japo walitumia mchezo wa nguvu.

Kwa upande wa Biashara Nahodha msaidizi Kauswa Bernad aliyeingia kipindi cha pili alisema wao walicheza kwa juhudi zao lakini wapinzani wao Alliance walikuwa wazuri kuliko wao kwa hiyo wanajipanga na michezo 10 iliyosalia.

Katika mchezo ulioshiuhudiwa na mashabiki wa kutosha jana magoli yaliyofungwa na Athanas Mdamula, Dickson Ambundo na Richard John aliyetoka benchi yalitosha kuwapa ushindi Alliance Schools katika kundi C na kurudi kileleni mwa kundi hilo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here