Home Kitaifa Kabla ya kuondoka Bongo, Msuva amezungumzia nafasi ya Yanga kutetea ubingwa na...

Kabla ya kuondoka Bongo, Msuva amezungumzia nafasi ya Yanga kutetea ubingwa na usajili wa Simba

4228
0
SHARE

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga Simon Msuva kupitia kipindi cha Sports Bar ndani ya Clouds TV amezungumza mambo mbalimbali kuhusu timu yake ya zamanikutetea ubingwa wa ligi, usajili wa Simba, nafasi ya wachezaji wa Tanzania kutoka nje ya nchi kwenda kucheza soka la kulipwa pamoja na vitu ambavyo anavi-miss akiwa Morocco.

Kuna wakati bado anajiona yupo Yanga

Kuna wakati bado najiona kama nipo Yanga, nina chembechembe zake kwa sababu nimecheza kwa muda mrefu na kupata mafanikio nikiwa pale, Yanga kwangu ni nyumbani.

Hali ilivyo sasa ndani ya Yanga

Yanga kwa sasa inachangamoto ndani na nje ya uwanja. Nadhani imeondokewa na wachezaji wengi wazuri kwa wakati mmoja mimi, Vicent Bossou, Haruna Niyonzima, Dida, ambao wote tulikuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza lakini imesajili wachezaji wengine naamini wakizoeana timu itafanya vizuri kwa sababu bado ni timu nzuri.

Matokeo yatafanya timu itulie hadi nje ya uwanja, mashabiki watatulia timu ikianza kufanya vizuri japo hata sasa bado haifanyi vibaya lakini ndio hivyo mashabiki wetu wanataka timu yao ishinde kila mechi.

Yanga bado ina nafasi ya kutetea ubingwa

Uwezekano wa kutetea ubingwa bado upo kwa sababu bado kuna mechi nyingi, hadi sasa hivi Yanga haipo kwenye nafasi mbaya kwa pointi walizonazo ukilinganisha na mechi walizocheza pamoja na pointi wanazozidiwa na timu inayoongoza ligi.

Bado mapema sana kuitoa Yanga kwenye mbio za kutetea ubingwa wao, ingekuwa mambo yapo hivi labda raundi ya pili hapo watu kutia mashaka kuhusu ubingwa ingekuwa sawa lakini kwa sasa bado nafasi wanayo.

Usajili wa Simba

Wanahitaji kitu ambacho hawajakipata kwa muda mrefu, wamefanya usajili wa kufuru hiyo inatosha kujua wanahitaji nini, wana timu nzuri. Simba wamesajili vizuri wanawachezaji wenye uzoefu na ligi pamoja na mechi za kimataifa.

Wachezaji wa tanzania kutoka nje

Inawezekana kutoka kwenda nje, wachezaji wanapaswa kujituma na kuweka nguvu kila kitu kinawezekana. Kufanya vizuri ukiwa ndani ndio kutakupa nafasi ya kusogea sehemu nyingine kwa hiyo wachezaji wanapaswa kufanya vizuri ndani kwanza ili kutengeneza nafasi ya kutoka nje.

Na-miss ugali

Nimemisi mishemishe za ‘kitaa’ kama unavyojua ukiwa nyumbani unakwenda kutembelea ndugu jamaa na marafiki mnakutana na kuzunguka maeneo tofauti lakini ni tofauti na unapokuwa kwenye nchi za watu hasa kama mimi bado mgeni.  Nime-miss pia misosi nikiwa kule sili ugali kwa sababu hakuna halafu hata wali wao upo tofauti na huku kwetu kutokana na aina ya mapishi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here