Home Kitaifa Goli la Ghana lililokataliwa vs Uganda linavyomkumbusha Machupa mwaka 2004 Stars kuchapwa...

Goli la Ghana lililokataliwa vs Uganda linavyomkumbusha Machupa mwaka 2004 Stars kuchapwa 3-0 ndani ya dakika 15

2181
0
SHARE

Mshambuliaji wa zamani wa Stars pamoja na klabu ya Simba Athumani Machupa amesema mambo ya mizengwe na figisu kwenye soka la Afrika yapo na ni kawaida sana kushuhudia timu moja ikionewa ili nyingine ifanikishe jambo lake inalolihitaji.

Machupa amesema hivyo baada ya kuzuka mjadala mkubwa duniani kote kuhusu goli la Ghana lililokataliwa wakati wa mechi yao ya kufuzu kuwania kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 zitakazofanyika Russia.

Mizengwe waliyokutana nayo Ghana wakati wanacheza ugenini dhidi ya Uganda inamkubusha Machupa mwaka 2004 wakati Stars ilipocheza ugenini dhidi ya Benin na kujikuta ikichapwa bao 3-0 ndani ya dakika 15 za kwanza.

“Nimebahatika kucheza hizi mechi za kufuzu kombe la dunia hizi figisufigisu unazoziona zimetokea kwenye mechi ya Uganda vs Ghana wenzetu Afrika Magharibi wanazitumia sana kupata matokeo. Siku zote usione hizi timu za Magharibi mwa Afrika zinakwenda kombe la dunia ukafikiri zote zinakwenda kihalali baadhi yao huwa zinalalamikiwa lakini inawezekana sisi huku huwa hatusikii kwa sababu hatuathiriki moja kwa moja.”

“Ukiangalia goli la Ghana lililokataliwa lilikuwa ni halali mimi nashangaa kwa nini limekataliwa ukizingatia kipindi hiki cha utandawazi kila kitu kinaonekana.”

“Figisu ambayo siwezi kuisahau nakumbuka ilikuwa ni 2004 tupo kwenye mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia tunatarajia kucheza na Benin ugenini. Tulipofika Benin tulikuta wananchi wameandaliwa kwa ajili ya maandano kuisapoti timu yao ya taifa na kuupa umuhimu mchezo dhidi yetu.”

“Nakumbuka hadi usiku wakati wa kulala brass band zilikuwa zinapiga nje ya hotel tuliyofikia usiku kucha kuamkia siku ya mechi. Nakumbuka siku ya mechi dakika ya tatu tu beki wetu akapewa kadi nyekundu, hadi kufikia dakika ya 15 tulikuwa tumefungwa 3-0 na magoli yote yalikuwa ni ya figisu.”

“Hatukuruhusiwa kuvuka mstari wa katikati katika kipindi chote tulichofungwa 3-0, ukijitahidi kuvuka hata ukigongana na mtu inapigwa firimbi faulo inaelekezwa kwetu.”

Tayari chama cha soka cha Ghana kimeshatuma malalamiko yake FIFA wakiomba mechi yao dhidi ya Uganda irudiwe kama walivyofanya kwenye mechi ya Afrika Kusini dhidi ya Senegal kufuta matokeo ya dakika 90 kutokana na makosa ya mwamuzi baada ya mwamuzi kuwapa Afrika Kusini penati isiyostahili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here