Home Kitaifa Baada ya mechi 3 tutajua nafasi na uimara wetu katika ligi, hatuna...

Baada ya mechi 3 tutajua nafasi na uimara wetu katika ligi, hatuna malengo zaidi ya ‘mechi kwa mechi’-Pluijm

2092
0
SHARE

Na Baraka Mbolembole

LICHA ya kikosi chake kupewa nafasi ya kufanya vizuri katika ligi kuu Tanzania Bara msimu huu, kocha wa timu ya Singida United, Mholland, Hans van der Pluijm anaamini bado mapema mno na michezo mitatu ijayo ambayo watacheza ugenini ndiyo itamwonyesha mwelekeo hasa wa timu yake ambayo imerejea VPL baada ya kupita miaka zaidi ya 13.

“Kwa sasa tuna mechi tatu ngumu za ugenini, baada ya hizi mechi tatu ndiyo tutajua uimara wetu na nafasi.” Anasema Hans wakati nilipofanya naye mahojiano Jumatatu hiii na kumuuliza anaonaje nafasi ya timu yake baada ya kucheza michezo mitano ya mwanzo ambayo wameshinda mitatu, satre moja na kupoteza mchezo mmoja.

Singida wapo katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi wakiwa na alama kumi, moja pungufu ya viongozi Simba, moja nyuma ya Mtibwa Sugar FC na Azam FC zilizofungana kwa pointi 11.

Hans ambaye ni mshindi mara mbili wa VPL akiwa na kikosi cha Yanga SC ataiongoza timu yake kuivaa Ruvu Shooting katika uwanja ambao hajawahi kuona timu yake ikicheza-Mabatini, Mlandizi. Shooting bado wanahangaika kusaka ushindi wa kwanza msimu huu baada ya kupoteza mchezo mmoja na kutoa sare nne wanakutana na Singida ambao wametoka kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC katika mchezo wa raundi ya tano .

“Tuna morali nzuri kwa sasa kwenye timu.” Anasema Hans ambaye alishinda VPL mara mbili mfululizo misimu ya 2014/15 na 2015/16 akiwa Yanga. Katika mazungumzo yangu na Hans nilimuuliza ni malengo gani hasa ambayo Singida United kama timu wamejiwekea msimu huu, naye alijibu vizuri kwa kuondoa dhana iliyoanza kujengeka kwa watu wengi kuwa kikosi chake kinatazama zaidi ubingwa kama lengo kuu.

“Msimu huu tunaangalia matokeo ya mechi kwa mechi na mwishoni mwa ligi tutaweza kujua nafasi yetu ni ipi tuliyofikia. Ni sawa tunataka kushinda, sitoweza kuwapa vijana wangu pressure zisiso na msingi, nalijua hilo kwa uzoefu wangu sio kila muda litasaidia, najua wachezaji watacheza kwa kujituma. Ligi ndo imeanza nadhani sitopenda kuongea sana.”

Singida United imekuwa ikitumia uwanja wa Jamhuri, Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani wakati huu Namfua Stadium ukiwa katika hatua za mwisho za matengenezo makubwa yanayoambana na uwekwaji wa ‘pitch’ ya kisasa. Katika michezo mitatu waliyocheza Jamhuri Stadium wamefanikiwa kushinda mara mbili na sare moja.

Nilimuuliza Hans kama kuna tatizo lolote kwa timu yake kucheza nje ya Singida wakati huu wakisubiri kukamilika kwa Namfua Stadium. “Uwanja ndiyo utaongea” anasema Hans na kuongeza, “Kwa sasa tunalazimika kuendana na hali hiyo (kucheza Dodoma.)

Sitotaka kulalamika sana kuhusu ubora wa viwanja. Kisaikolojia haitomsaidia mtu na tuna viwanja dizaini hii vingi. Kikubwa ni kuweka mkazo na kutazama zaidi katika mchezo kuliko viwanja. Inatakiwa kucheza, ni kwa timu zote sio rahisi.”

Hans anakumbukwa sana kwa vikosi vyake vilivyokuwa vikicheza mchezo wa kushambulia sana katika timu ya Yanga kati ya mwaka 2014 hadi 2016 alipoondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mzambia, George Lwandamina.

“Hakuna chochote ninachokimisi kwa sasa Yanga, hakuna tatizo.” anamaliza kusema Hans.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here