Home Kimataifa Salah amekata kiu ya Misri iliyodumu kwa miaka 27

Salah amekata kiu ya Misri iliyodumu kwa miaka 27

3338
0
SHARE

Mahamed Salah alikwamisha kambani mkwajun wa penati dakika za za usiku kuiwezesha Misrei kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia baada ya kusubiri kwa miaka 27 tangu walipofuzu kwa mara ya mwisho.

Salah alifunga magoli yote ya Misri kwenye ushindi wa 2-1 nyumani dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu kwa upande wa Afrika.

Misri inafuzu kwenda fainali za kombe la duni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990 huku mkwaju wa penati ya mguu wa kushoto wa Salah katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza ikaleta ushindi uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wan chi nzima.

Ilikuwa ni furaha isiyo na mfano kwa wakazi wa Misri wanaokaribia milioni 100 ambao wamesubiri kwa muda mrefu kufuzu michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.

Unaambiwa ushindi huo umepelekea maelfu ya mashabiki kujazana kwenye mita ya Misri wakisherekea huku wakipeperudha bendera za taifa lao. Katikati ya jiji la Cairo helicopter ya kijeshi ilikuwa ikidondosha mamia ya bendera za nchi hiyo kwa mashabiki waliokuwa barabarani wakishangilia kwenye sehemu maarufu inayofahamika kwa jina la Tahrir square.

Misri imekuwa nchi ya pili kufuzu kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 2018 nchini Russia baada ya Nigeria kujihakikishia nafasi siku ya Jumamosi. Mataifa mengine matatu ya Afrika yatakata tiketi zao mwezi ujao kwenye mechi za kuwania kufuzu.

Salah huenda alidhani ameshaisaidia Misri kushinda mchezo huo kwa goli lake la dakika ya 63 lakini Misri walistushwa na bao la kusawazisha la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya Arnold Bouka Moutou kutandika volley na kusawazisha dakika ya 86.

Mahmoud Hassan aliyeingia akitokea benchi aliangushwa kwenye box dakika mbili za nyongeza na Salah ambaye ndio star wa Misri akaifunga bao la ushindi kwa kiki ya penati.

Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000 ambao ni uwanja wa jeshi uliopo kwenye jiji la Alexandriasababu za kupeleka mechi hiyo kwenye uwanja wa jeshi ni hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo kwa zaidi ya miaka sita iliyopita.

Athari za masuala ya kisia nchini Misri yameathiri pia soka la nchi hiyo pia, ikiwa na historia ya kushinda taji la Afrika mara saba, Misri imeshindwa kufuzu fainali tatu za mataifa ya Afrika kwa misimu mitatu mfululizo tangu mwaka 2012-2015 kabla ya kurejea kwenye fainali za mwaka huu

Kocha raia wa Argentina Hector Cuper amekiongoza kikosi cha Misri kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwezi February mwaka huu na kupoteza mbele ya Cameroon. Kuiongoza Misri kufuzu fainali za kombe la dunia ni mafanikio makubwa kwa kocha huyo licha ya taifa hilo kuwa na historia kubwa kwenye soka la Afrika.

Misri imefanikiwa kushiriki mara mbili fainali za kombe la dunia 1934 na 1990 lakini 2018 itakuwa ni mara yao ya tatu. Misri itamaliza juu ya Kundi E ikiwa imejihakikishia nafasi yake kwenye fainali za kombe la dunia huku ikiwa na mechi moja mkononi itakayochezwa mezi ujao dhidi ya Ghana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here