Home Kimataifa Iceland wafuzu kombe la dunia kwa mara ya kwanza

Iceland wafuzu kombe la dunia kwa mara ya kwanza

3946
0
SHARE

Kwa mara ya kwanza Iceland wamefudhu kombe la dunia na huku wakiongoza kundi lao la I baada ya hii leo kuibuka kidedea kwa bao 2 kwa 0 Kosovo kwa mabao yaliyofungwa hii leo na Sigurdsson na J Gudmundsonn.

Antonio Candreva alifunga bao moja na kuisaidia Italia kuibuka kidedea dhidi ya Albania huku Hispania ambao wameshatangulia kombe la dunia wakiichapa Israel moja kwa sifuri.

Crotia waliibuka kidedea kwa bao mbili kwa sifuri kwa mabao ya Andrej Kramaric huku mchezo mwingine katika Group I Turkey walikwenda suluhu ya bao mbili kwa mbili dhidi ya Finland.

Katika Group D timu ya taifa ya Wales wakiwa nyumbani walikubali kupigwa bao moja kwa nunge kutoka Ireland bao likifungwa na James McClean, huku Serbia nao wakiwa nyumbani wakaichapa Georgia moja kwa nunge bao la Prijovic.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here