Home Kitaifa Yanga imeshindwa kupata ushindi kwa timu ya daraja la kwanza

Yanga imeshindwa kupata ushindi kwa timu ya daraja la kwanza

8018
0
SHARE

Yanga wamebanwa na KMC na kulazimishwa suluhu kwenye mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu ilichezwa usiku wa leo Jumapili October 8, 2017 kwenye uwanja wa Azam Complex.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga, wametumia mechi hiyo kuwapa fursa wachezaji wengi ambao wamekuwa hawaanzi kwenye kikosi cha kocha George Lwandamina.

KMC ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara imetoa ushindani wa kutosha kwa Yanga kutokana na kiwango chao bora walichokionesha wakiwa chini ya kocha Fred Minziro ambaye aliwahi kuwa kocha wa Yanga miaka kadhaa iliyopita.

Kwa upande wa Yanga mechi hiyo pia ilikuwa ni muhimu nje ya uwanja kwa sababu wamelenga kutumia mapato ya mchezo huo kwa ajili ya kukarabati uwanja wao wa Kaunda.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here