Home Kimataifa Super Egles wawa Waafrika wa kwanza kukata tiketi ya Urusi

Super Egles wawa Waafrika wa kwanza kukata tiketi ya Urusi

3685
0
SHARE

Tangu karne ya 21 ianze, timu ya taifa ya Nigeria haijawahi kupoteza mchezo wa kufudhu kwenda kombe la dunia katika ardhi yao ya nyumbani, wamesuluhu mara tatu zilizobaki ni ushindi.

Sasa wanakuwa taifa la kwanza kutoka Africa kwenda Urusi kuliwakilisha bara hili katika michuano ya kombe la dunia huku bao la Alxendre Iwobi likipeleka furaha Lagos.

Hii ni mara ya 6 kwa Super Eagles kucheza kombe la dunia  kwani mwaka 1994, 1998 na 2014 walishiriki wakiishia raundi ya pili huku mwaka 2002 na 2010 wakiishia hatua ya makundi.

Taifa jingine lililofudhu hiyo jana kwa ajili ya kombe la dunia mwakani ni Costa Rica ambapo bao la muda wa lala salama la Kendall Waston lilishuhudia Costa Rica wakienda kombe la dunia kwa mara ya 5.

Kabla ya mchezo wa jana kati ya Sweden na Luxembourg, mshambuliaji wa Sweden Marc Berg hakuwahi kufunga goli zaidi ya moja lakini jana akaweka nne katika ushindi wao wa mbak 8 kwa 0.

Ushindi wa jana wa Ubelgiji wa mabao manne kwa matatu dhidi ya Bosnia unawafanya Wabelgiji kutopoteza hata mechi moja tangu mwaka 2009 huku wakiwa wamefunga jumla ya mabao 57 na kuruhusu 10 tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here