Home Kimataifa Ghana waiomba FIFA kuwatendea haki baada ya kuonewa dhidi ya Uganda

Ghana waiomba FIFA kuwatendea haki baada ya kuonewa dhidi ya Uganda

6696
0
SHARE

Jana kulipigwa michezo mingi kwa ajili ya kufudhu fainali za kombr la dunia, lakini kati ya mchezo uliovuta hisia za wana Afrika Mashariki ni mchezo kati ya wawakilishi pekee wa uknada huu Uganda waliokipiga dhidi ya Ghana.

Mchezo ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana lakini tukio lililovuta hisia za wengi lilikuwa goli la Raphael Dwamena ambalo lilifungwa kwa mpira wa rebound lakini muamuzi akalikataa.

Katika picha za video inaonesha Dwamena alikuwa katika eneo ambalo sio la kuotea wakati akifunga bao hilo na sasa chama cha soka nchini Ghana kimeamua kumfungulia mashtaka muamuzi huyo.

GFA wameamua kwenda FIFA kumshitaki muamuzi Daniel Bennet na msaidizi wake Eldrick Adelaide kwa kile wanachodai kwamba alishindwa kuumudu mchezo na alikuwa sababu ya wao kukosa alama 3.

Sii hivyo tu bali GFA wanasema ukiacha bao hilo la wazi lakini pia muamuzi huyo aliwanyima penati katika kipindi cha pili baada ya Frank Acheampong kuangushwa katika eneo la kumi na nane.

Ghana walinyimwa mabao mawili ambayo yote yanaonekana hayakuwa na matatizo hukubpia wakinyimwa penati na sasa wameiomba FIFA kupitia tena mchezo huo na kutenda haki bila uoga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here