Home Kimataifa Baada ya goli la Ghana kukataliwa vs Uganda, Gyan amesema nchi yake...

Baada ya goli la Ghana kukataliwa vs Uganda, Gyan amesema nchi yake ni dhaifu

17409
0
SHARE

Mara baada ya mchezo kumalizika kwa matokeo ya bila kufungana kati ya Unganda dhidi ya Ghana wakati timu hizo zikipambana kuwania kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Russia, nahodha The Black Stars Asamoah Gyan amesema Ghana ni lazima wapinge kuhugoli lao lililokataliwa na mwamuzi.

Katika mchezo huo, Ghana walifunga magoli mawili lakini yote yakakataliwa huku wakinyimwa pia mkwaju wa penati na mwamuzi Daniel Bennett aliyekuwa akisaidiwa na washika vibendera Eldrick Adelaide na Steve Marie .

“Inawezekanaje goli kama hili kukataliwa. Lazima tupinge katika hili, Ghana ni dhaifu katika kupinga. Kila kitu ni “Fama Nyame”. Nimechukizwa” ameandika Gyan kwenye ukurasa wake wa instagram (asamoah_gyan3).

Goli lililozua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka ni lile lililofungwa dakika za majeruhi (dakika nne za nyongeza) ambapo Raphael Dinamena alikwamisha mpira kambani uliotemwa na golikipa wa Uganda Dennis Onyango lakini lakini kibendera cha Jonathan Steve Marie kilikuwa juu kuashiria ni offside.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here