Home Kimataifa Qatar mashakani kuandaa kombe la dunia 2022

Qatar mashakani kuandaa kombe la dunia 2022

2474
0
SHARE

Mashindano ya kombe la mwaka 2022 yametawaliwa na wasiwasi mkubwa kushindikana kufanyika Qatar. Baada ya suala la rushwa kuonekana kuzimwa sasa inaonekana kumekuja tishio jipya.

Qatar ipo katika mgogoro mkubwa wa masuala ya kisiasa ndani ya nchi yao huku uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani ukiwa katika hali ambayo sio nzuri kiasi cha kutishia uandaaji wa mashindano hayo.

Ripoti iliyotolewa na shirika moja kubwa la habari barani Ulaya imedai kwamba mgogoro wa Kidiplomasia unaoendelea Qatar unaweza kupelekea taifa hilo kushindwa kuandaa michuano hiyo mikubwa.

Vilevile Qatar hadi sasa haijakamilisha miradi mikubwa mingine ikiwemo wa miundombinu huku ikihitajika kiasi cha £153b ili kukamilisha, kiasi ambacho kinaonekana ni kikubwa sana na inawezekana washindwe kukamilisha miundombinu hiyo kwa wakati.

Habari ya Qatar kupokonywa uenyeji wa mashindano haya ni habari nzuri kwa taifa la Australia na Uingereza ambapo mataifa hayo mawili yanaonekana kupewa nafasi kubwa kuandaa michuano hiyo kama Qatar wakishindwa.

Nchini Qatar hadi sasa ni uwanja mmoja tu wa Khalifa Stadium ulioko Doha ndio ambao umekamilika huku viwanja vingine vikiwa vinasua sua na inasemekana wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi katika wakati mgumu sana.

Shirika moja la haki za wanaadamu limeeleza kuwa wafanyakazi wengi wamefariki nchinjli Qatar kutokana na hali ya hewa na kazi ngumu ya ujennzi wa viwanja ripoti ambayo serikali ya Qatar imeiita Kichekesho.

Qatar inashutumiwa na mataifa ya jirani kwamba imekuwa ikunga mkono masuala ya ugaidi na hivyo kuwekewa vikwazo na majirani zakr ikiwemo nchi ya Saudi Arabia ambayo imekataa raia wa Qatar kuingia nchini mwao.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa taifa kupokonywa michuano ya kombe la dunia ambapo mwaka 1986 masuala ya kiuchumi yalishuhudia Colombia wakipokonywa michezo hiyo na kukabidhiwa Mexico.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here