Home Kimataifa Ndoto za Mali kushiriki kombe la dunia zakaribia kuzima

Ndoto za Mali kushiriki kombe la dunia zakaribia kuzima

4078
0
SHARE

Na Bosha Nyanje.

Mali wameendelea kupoteza ndoto za kucheza kombe la Dunia mwakani baada ya kulazimishwa suluhu kwenye uwanja wa nyumbani kwenye mchezo wao wa kundi C dhidi ya Ivory Cost.

Mali ambao wana alama 3 wanaendela kuburuza mkia kwenye kundi C ambalo linaongozwa na Ivory Cost wenye jumla ya alama 8 baada ya Michezo 5.

Katika mchezo huo Mali walionekana kucheza kwa kujiamini na kumili mpira kipindi cha kwanza Licha ya kushindwa kuipenya ngome ya ulinzi ya Ivory Cost inayoongozwa na Erick Baily anayecheza Manchester United.

Mali licha ya kupata pigo dakika ya 40 baada ya staa wao Adama Traore kuumia na nafasi yake kuchuliwa na Mouse Djenepo ambayo juhudi zake hazikuza matunda katika mchezo huo 

Mali ambao walipoteza nafasi ya kuongoza baada ya mkwaju wa adhabu ndogo mnano dakika ya 27 kuchezwa vizuri na kipa wa Ivory Cost Gbohouo 

Vikosi vilivyoanza kwenye mchezo huo ni 

Mali : Diarra, Wagué, Traoré, Koné, Fofana, Doumbia, Samassekou,Diarra,Bissouma,Niane, Traore

Ivory Cost: Gbohouo, Aurier,Kanon,Bailly,Konan,Dié,Gbamin,Kessié, kodjia, Cornet, Assalé

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here