Home Kitaifa Msuva amenusuru rekodi ya Mayanga kuchafuliwa

Msuva amenusuru rekodi ya Mayanga kuchafuliwa

5071
0
SHARE

Bao pekee la kusawazisha lililofungwa na Simon Msuva limemuokoa kocha wa Stars Salum Mayanga kupoteza mechi ya kwanza kwenye uwanja wa nyumbani. Stars imelazimisha matokeo ya sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Malawi kwenye mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA.

Mayanga tangu amekuwa kocha wa Stars amecheza mechi moja kwenye ardhi ya Afrika Kusini alipofungwa 4-2 na Zambia kwenye nusu fainali ya mashindano ya COSAFA.

Hadi sasa Mayanga ameiongoza Stars kucheza mechi 13, maeshinda michezo sita (6), sare sita (6) huku akipoteza mchezo mmoja tu.

Tanzania 2-0 Botswana

Tanzania 2-1 Burundi

Tanzania 1-1 Lesotho

Tanzania 2-0 Malawi

Angola 0-0 Tanzania

Tanzania 1-1 Mauritius

Afrika Kusini 0-1 Tanzania

Zambia 4-2 Tanzania

Tanzania 0-0 Lesotho (Tanzania ilishinda kwa penati 4-2)

Tanzania 1-1 Rwanda

Rwanda 0-0 Tanzania

Tanzania  2-0 Botswana

Tanzania 1-1 Malawi

Msuva ameisawazishia Stars dakika ya 57 kipindi cha pili baada ya kupiga kona na kuzama kambani moja kwa moja baada ya beki wa Malawi kuuokoa mpira ambao tayari ulishavuka mstari wa goli.

Goli la Malawi lilifungwa na Ngambi Robert ambaye ni nahodha ikiwa ni dakika ya 35 kipindi cha kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here