Home Kimataifa Messi, CR7, Bale, Buffon, Sanchez na mastaa wengine ambao huenda wakaangalia World...

Messi, CR7, Bale, Buffon, Sanchez na mastaa wengine ambao huenda wakaangalia World Cup kwenye TV

10822
0
SHARE

Hatua ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 inakaribia kumalizika, lakini kuna uwezekano mkubwa wachezaji wenye majina makubwa wakaikosa michuano hii mikubwa zaidi duniani.

Argentina: Lionel Messi, Sergio Aguero, Angel Di Maria, Mauro Icardi, Paulo Dybala, Gonzalo Higuain, Javier Mascherano

Listi ya vipaji vilivyopo chini ya Jorge Sampaoli inatisha, lakini bado Argentina ipo kwenye matatizo makubwa. Kombr la dunia bila uwepo wa Lionel Messi ni jambo litakalokuwa pigo kwa mashindano, lakini pia kuna wachezaji wengine wa kiwango cha dunia ambao watakosekana kwenye michuano hiyo

Argentina wanahitaji kushinda mchezo wa ugenini vs Ecuador — ambapo wameshinda mara 1 tu tangu mwaka 1960 — endapo watafanikiwa kushinda mchezo huo basi huenda wakapata nafasi ya kucheza play off dhidi ya New Zealand. Au huenda wakafuzu moja kwa moja ikiwa Brazil itafanikiwa kuifunga Chile ugenini.

Portugal: Cristiano Ronaldo

Mshindi wa Ballon d’Or, wa mara mbili mfululizo, mshindi wa Champions League mara mbili mfululizo na mshindi wa kombe la Euro, huyu pia huenda tukamkosa mwakani pale Russia. Ureno wanashika nafasi ya pili kwenye kundi lao nyuma ya Switzerland kwa pointi 3. Mataifa haya mawili yanakutana jijini Lisbon jumanne ijayo, na ikiwa Ureno hawatoshinda basi itabidi wapitie kwenye play off tena safari hii.

Chile: Alexis Sanchez, Arturo Vidal

Goli la dakika ya 85 la Alexis Sanchez dhidi ya Ecuador liliweka hai matumaini ya Chile kufuzu, lakini mshambuliaji huyo wa Arsenal anahitaji kufanya makubwa zaidi ili kuhakikisha timu yake inapata ushindi dhidi ya Brazil jumanne ijayo. Endapo watapata sare na Argentina ikapoteza vs Ecuador basi watacheza dhidi New Zealand katika mtoano.

Italy: Gianluigi Buffon

Baada ya kupangwa katika kundi na Spain, kulikuwa na wasiwasi wa moja kwa moja kwamba mmoja wa vigogo wa soka ulaya atakosa kombe la dunia au ataishia kufuzu kupitia play off na sasa inaonekana wazi Gianluigi Buffon na wenzake itawabidi kupitia hatua ya mtoano baada ya kushindwa kuwapiku mabingwa wa dunia wa 2010. Buffon ameshatangaza kwamba michuano ijayo ya dunia itakuwa ya mwisho – Je ndoto yake itatimia?

Netherlands: Arjen Robben

Kuporomoka kwa soka la Uholanzi kunaendelea, na nyota wa Bayern Munich huenda akazikosa fainali za kombe la dunia. Robben atahitaji kuiongoza timu yake kushinda mechi 2 zilizobaki wiki hii na wakiiombea Sweden kubotonga ili waweze hata kupata nafasi ya kucheza play off.

Wales: Gareth Bale

Huku Bale akiwa nje kwenye mechi zote mbili zilizobaki za hatua ya makundi dhidi ya Georgia na Republic of Ireland kutokana na maumivu, nafasi za Wales kuikosa michuano ya dunia bado ipo.

Baada ya ushindi wa leo vs Georgia, Wales wanahitaji kushinda mechi ijayo pia ili kuweza kupata nafasi ya kucheza katika play off.

United States: Christian Pulisic

Kiungo wa Borussia Dortmund ni mmoja kati ya viungo bora kabisa wanaochipukia katika ulimwengu wa soka, na soko litapanda zaidi akicheza katika Kombe la dunia. Lakini USA wapo nje za pointi za kufuzu moja kwa moja na endapo watapoteza mchezo dhidi ya Panama basi nafasi pekee watakayokuwa nayo ni kufuzu kwa kucheza kwenye Play Off.

Lakini US wanafahamu kabisa ikiwa watafanikiwa kushinda mechi mbili zilizobaki basi watafuzu moja kwa moja kwenda Russia..

Gabon: Pierre-Emerick Aubameyang

Uamuzi wa Pierre-Emerick Aubameyang wa kutokucheza mchezo muhimu dhidi ya Ivory Coasta mwezi uliopita, ambao walipoteza 3-0, unamaanisha kwamba wana nafasi ndogo ya kupata nafasi ya kwenda Russia 2018. Kwa hali ilivyo Ivory Coasta wanaongoza kundi lao watafuzu na dunia itakosa kumuona mmoja wa washambuliaji hatari duniani katika michuano mikubwa ya dunia.

Senegal: Sadio Mane

Winga wa Liverpool ni mmoja ya wachezaji bora kabisa kutoka katika hara la Afrika anayetamba katika EPL, lakini yeye ni mmoja ya mafundi ambao huenda wasikanyage Russia mwakani. Senegal bado wana mchezo wa kiporo dhidi ya South Africa ambao unatakiwa kurudiwa. Na ikiwa watafanikiwa kushinda mechi zote 3 zilizobaki basi watafuzu, wasipofanya hivyo basi wakati wa kiangazi ujao watakuwa kwenye mapumziko.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here