Home Kitaifa Kocha wa Malawi kataja wachezaji wawili wa Stars waliosumbua

Kocha wa Malawi kataja wachezaji wawili wa Stars waliosumbua

6323
0
SHARE

Baada ya mchezo wa kirafiki kati ta Taifa Stars dhidi ya Malawi kumalizika, kocha wa Malawi Ron van Geneugden amewataja Mbwana Samatta anaecheza barani Ulaya katika klabu ya KRC Genk pamoja na kiungo mshambuliaji wa Simba Ramadhani Kichuya kwamba ndio wachezaji ambao walikuwa hatari zaidi kwao

Geneugden amewataja Samatta na Kichuya mbele ya waandishi wa habari kwamba walikuwa wasumbufu uwanjani hususan katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili.

“Jezi namba 10 (Mbwana Samatta) na jezi namba 16 mara nyingi alikuwa anacheza¬† upande wa kushoto (Ramadhani Kichuya) walikuwa hatari kwetu hasa baada ya kurudi kutoka mapumziko”

Kocha huyo pia amelalamikia maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na mwamuzi wa kati wa mchezo huo Israel Mjuni ambaye alimwamuru kuondoka kwenye benchi la ufundi baada ya kuonekana akilalamikia maamuzi yake kwa fourth official Elly Sasii.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here