Home Kimataifa Wakiwa kwenye vita ya miaka 6 – Syria kujifuta machozi na kufuzu...

Wakiwa kwenye vita ya miaka 6 – Syria kujifuta machozi na kufuzu kombe la Dunia?

3030
0
SHARE

Wakati miji mbalimbali ya nchi hiyo ikiwa katika hali mbaya na mamilioni ya wananchi wake wakiwa wanapigika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, Syria wanapigana kufanikisha ndoto ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia 2018.

Wakiwa hawapewi nafasi kabisa, kikosi cha timu ya taifa ya Syria kinachoshika nafasi ya 75 ya ubora duniani, kimeushangaza ulimwengu wa soka duniani kwa kuwavimbia na kutoka sare na timu kama Korea ya Kusini na Iran, wamewafunga China, Qatar na Uzbekistan – matokeo ambayo yaliwapa nafasi ya pili katika kundi lao na nafasi ya kucheza play-off.

Wasyria wanaojulikana kwa jina la “Qasioun Eagles” walipata taabu kukabiliana na michezo ya kundi lao – wakicheza mechi zao za nyumbani katika ardhi ya Oman na Malaysia.

Leo jioni wamepata sare dhidi ya Australia, wametoka sare ya 1-1 katika mchezo uliopigwa nchini Malaysia. Sasa mchezo huo utarudiwa nchini Australia na mshindi atacheza dhidi ya mshindi wa 4 wa kundi la CONCACAF qualifiers, ambaye huenda akawa Panama, Honduras au hata Marekani.

Mpaka kufikia hapa Syria wamepambana kuvuka vikwazo vyote, nchi yao ikiwa imegubikwa na vita ambayo imeshachukua uhai wa watu 470,000 na wengine mamilioni wakiwa hawana makazi ya kuishi – kwa mujibubwa shirika la haki za binaadamu la Uingereza ambalo limesema mwezi September umekuwa mwezi ambao damu imemwagika zaidi katika vita hiyo iliyodumu kwa miaka 6 sasa.

Vikosi vya kijeshi vya Syria – vinavyomsapoti Rais Bashar al-Assad, sasa vinashikilia maeneo mengi ya mjini kufuatia mapigano ya miaka 4 katika eneo la Aleppo, mji wa pili kwa ukubwa wa nchi hiyo – na sasa vikosi vya jeshi vinajiandaa kwa pambano la mwisho dhidi ya kikundi cha Islamic State (ISIS) kwa ajili ya kuchukua eneo la Deir Ezzor.

Rais Assad, ambaye amekuwa akituhuhumiwa kuhusika makosa ya jinai ya kivita – anaripotiwa kuwa shabiki mkubwa wa Qasioun Eagles, jambo limepelekea watu kadhaa kuhisi kama huenda mafanikio ya timu ya taifa yakatumika kisiasa.

Lakini wachezaji wa Syria wanasema hakuna anayejihusisha na masuala ya siasa.

“Hatujihusishi kabisa na masuala ya siasa,” anasema mshambuliaji Firas Khatib alipokuwa akiongea na gazeti la Times. “Tunajituma kuhakikisha tunamwakilisha kila raia wa Syria.”

Nafasi ya kuweza kufuzu kucheza kombe la dunia imekuwa jambo lenye hisia kubwa kwa Wasyria ambao wengi wao wanaugulia maumivu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Tarehe 10, mwezi huu – mamilioni ya wananchi wa Syria watasimama kwa dakika 90 kuiombea kheri timu yao katika mchezo wa marudiano dhidi ya Australia ili kuamua timu itakayopata nafasi ya kwenda kucheza na mshindi kutoka CONCACAF.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here