Home Kitaifa Top 3 ya manahodha wa muda mrefu ligi kuu Tanzania bara

Top 3 ya manahodha wa muda mrefu ligi kuu Tanzania bara

8397
0
SHARE

Katika timu 16 za VPL, kuna jumla ya manahodha 16 (ukiachana na wasaidizi) ambao ni viongozi wa wachezaji wenzao uwanjani nanje ya uwanja pia. Manahodha wanne kati 16 ndio wamedumu kwa muda mrefu kwenye timu zao katika nafasi hiyo.

Ieleweke manahodha wanaozunvumziwa hapa ni wale ambao bado wapo kwenye nafasi hiyo hadi sasa (haihusishi waliokuwa manahodha timu A lakini sasa wapo B mfano John Bocco au Juma Kaseja).

Shabani Nditi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, George Kavila na Laurian Mpalile ni manahodha waliodumu kwa muda mrefu katika vilabu vyao wakiwa katika nafasi hiyo.

Nadir Haroub Cannavaro (Yanga)

Nahodha wa Yanga na zamani timu ya taifa, Cannavaro alikabidhiwa kitambaa cha unahoha mwaka 2013 mara baada ya nahodha wa wakati huo Shadrack Nsajigwa kustaafu kuitumikia klabu hiyo.

Cannavaro amekuwa nahodha wa Yanga kwa miaka minne mfululizo lakini siku za hivi karibuni hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza hivyo mara nyingi kitambaa cha unahodha kimekuwa kikivaliwa na Thabani Kamusoko na Kelvin Yondani ambao ni wasaidizi wake.

George Kavila (Kagera Sugar)

Mkongwe wa Kagera na ligi kuu Tanzania bara, alijiunga na Kagera Sugar mwaka 2009, mwaka 2013 akateuliwa kuwa nahodha wa timu hiyo akirithi mikoba ya Martin Muganyizi ‘Mwalala’ aliyekuwa nahodha kabla ya Kavila.

Kavile amekuwa nahodha kwa miaka minne hadi sasa akiwa mfano wa kuigwa ndani ya uwanja na nje ya uwanja si na wachezaji wa Kagera pekee bali wachezaji wote wa Tanzania kutokana na nidhamu yake ya hali ya juu pamoja na kujituma kwa ajili ya timu yake.

Shabani Nditi (Mtibwa Sugar)

Baba mwenye mtibwa yake aliyedumu kwenye ligi kwa muda mrefu, lakini anavyocheza huwezi kudhani kama ameanza kulitumikia soka kwa muda mrefu, bado anacheza kwenye kikosi cha kwanza cha Mtibwa Sugar  na kutoa changamoto ya kweli kwa wachezaji vijana katika kuwania nafasi.

Ameanza kuitumikia mtibwa kama nahodha tangu mwaka 2008, huyu ndio nahodha wa muda mrefu kwenye ligi ambaye bado anavaa kitambaa cha uongozi hadi leo. Miaka tisa (9) amekuwa katika nafasi hiyo huku akisaidiwa na baadhi ya wachezaji ambao wengine wameshaondoka na kumwacha kwenye timu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here