Home Kimataifa Hispania waenda kombe la dunia kwa mara ya 11 mfululizo

Hispania waenda kombe la dunia kwa mara ya 11 mfululizo

2601
0
SHARE

Timu ya taifa ya Hispania imewafuata Uingereza katika michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3 dhidi ya Albania huku Rodrigo, Isco na Thiago Alcantara wakiifungia Hispania.

Italia walipata suluhu na Macedonia ya bao moja kwa moja huku Giorgio Chiellini akiifungia Italia na Aleksandar Trakovski akiisawazishia Macedonia,huku Tom Lawrance akoofungia bao pekee Wales dhidi ya Georgia.

Luca Modric akiichezea Crotia mchezo wake wa 100 walipata suluhu dhidi ya Iceland huku Mario Mandzukic akiifungia Crotia na bao la Iceland likiwekwa kimiani na Pyry Soyr.

Nemanja Matic aliifungia Serbia bao moja kati ya mawili lakini akashindwa kuiokoa kupigwa bao 3 kwa 2 kutoka kwa Austria huku mabao ya Austria yakifungwa na Guido Bugstaller, Marko Arnautovic na Louis Schaub.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here