Home Kimataifa Andres Iniesta awa mchezaji wa kwanza kusaini mkataba wa milele

Andres Iniesta awa mchezaji wa kwanza kusaini mkataba wa milele

7224
0
SHARE

Tarehe 6 mwezi October mwaka 1996 ndio kwa mara ya kwanza Andres Iniesta alianza kuitumikia Barcelona, kuanzia hapo kilichoendelea ni historia akibeba makombe 30 katika michezo 639.

Kumekuwa na habari nyingi za hivi karibuni zikimuhusisha Iniesta ambapo ilisemekana kwamba kiungo huyo anaweza asimwage wino katika klabu hiyo kutokana na mazungumzo ya mkataba kuchukua mda mrefu huku mkataba alionao kuisha mapema mwakani.

Baada ya habari hizo hii leo Andres Iniesta amewaziba watu midomo kabisa baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kusaini mkataba wa maisha, inamaanisha Iniesta amesaini mkataba utakaomuweka Barca hadi anastaafu soka.

Iniesta mwenye miaka 33 kwa sasa, alikuwepo Barcelona tangu akiwa na miaka 12 lakini alikuwa akiichezea timu ya vijana na ilipofika mwaka 2002 Mhispania huyo kwa mara ya kwanza alichezea timu ya wakubwa.

Klabu ya Barcelona imesema kwa miaka 118 ya Historia ya klabu hiyo wasingependa kuona kizazi cha dhahabu kama cha wakiana Iniesta kupotea kirahisi na ndio maana haikuwa ngumu kumpa mkataba wa milele na usiokuwa na mwisho.

Andres Iniesta baada ya kusaini mkataba huo amesema kwamba kubaki hapo ndio ilikuwa ndoto yake na pamoja na miaka 33 aliyonayo lakini hajawahi kuwaza kufanya kitu kingine zaidi ya kubaki Nou Camp.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here