Home Kitaifa Timu 3 hazijapata ushindi tangu kuanza kwa VPL 2017/18

Timu 3 hazijapata ushindi tangu kuanza kwa VPL 2017/18

4409
0
SHARE

Ikiwa tayari kila timu imeshacheza michezo mitano ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu, timu tatu kati ya 16 bado hazijaonja ladha ya ushindi katika ligi hadi sasa.

timu tatu kongwe kwenye ligi (Ruvu Shooting, Majimaji pamoja na Kagera Sugar) bado zinapambana kupata ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa msimu huku matokeo ya sare yakiwa ni ushindi wao hadi sasa.

Ruvu Shooting

Ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo ikiwa na pointi nne baada ya michezo mitano. Shooting wametoka sare katika mechi nne huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja ambao waliambulia kichapo cha goli 7-0 kutoka kwa Simba kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi.

Wamecheza mechi tatu ugenini wamefungwa mchezo mmoja na kutoka sare mechi mbili, mechi zao mbili za uwanja wa nyumbani wamelazimishwa sare.

 • Simba 7-0 Ruvu Shooting
 • Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
 • Lipuli 0-0 Ruvu Shooting
 • Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar
 • Ruvu Shooting 1-1 Njombe Mji

Majimaji 

Timu nyingine ambayo inasuasua kwenye ligi licha ya kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa kwenye ligi kama Jerry Tegete, Danny Mrwanda, Tumba Sued na wengine lakini hali yao sio nzuri hadi sasa wakiwa bado wanatafuta ushindi wa kuanzia.

Majimaji imepoteza mechi mbili na kutoka sare michezo mitatu. imefungwa mechi moja ugenini, ikafungwa pia mechi nyingine uwanja wa nyumbani kisha ikapata sare mbili nyumbani na moja ugenini. Katika mechi tano walizocheza hadi sasa, mechi tatu wamecheza kwenye uwanja wao wa nyumbani huku nyingine mbili wakiwa jijini Mbeya.

Majimaji ipo nafasi ya 14 kwa pointi zake tatu sawa na Stand United ambayo ipo nafasi ya 15, timu hizo zinatofautishwa na wastani wa magoli.

 • Mbeya City 1-0 Majimaji
 • Tanzania Prisons 2-2 Majimaji
 • Majimaji 1-1 Yanga
 • Majimaji 0-1 Njombe Mji
 • Majimaji 0-0 Kagera Sugar

Kagera Sugar

Ilimaliza nafasi ya tatu msimu uliopita nyuma ya Simba waliokuwa washindi wa pili na Yanga ambao walitwaa taji la ligi kwa msimu huo.

Timu hii pia ilitoa kocha bora wa msimu (Mecky Maxime) ambaye yupo na timu hadi sasa, mchezaji bora chipukizi (Mbaraka Yusuph) kwa sasa amejiunga na Azam pia ilitoa golikipa aliyekuwa anawania tuzo ya golikipa bora wa msimu (Juma Kaseja) ambaye ameendelea kuwepo kwenye kikosi cha Kagera Sugar hadi sasa.

Kagera imepoteza mechi tatu kati ya tano ilizocheza hadi sasa na kutoka sare katika michezo miwili. Imefungwa mechi mbili na kutoka sare mchezo mmoja katika mechi tatu za ugenini, katika michezo miwili ya nyumbani imefungwa mmoja na mwingine kutoka sare.

Ipo katika nafasi ya mwisho (16) kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi mbili zinazotokana na sare mbili.

 • Kagera Sugar 0-1 Mbao
 • Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
 • Azam 1-0 Kagera Sugar
 • Stand United 1-0 Kagera Sugar
 • Majimaji 0-0 Kagera Sugar

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here